WINGA Arjen Robben amesema alimkatalia kocha wake wa timu ya taifa, Louis van Gaal wazo la kujiunga na klabu yake mlya, Manchester United.
Van Gaal ameipa Uholanzi nafasi ya tatu katika Kombe la Dunia baada ya jana kuifunga mabao 3-0 Brazil na baada ya hapo, Robben amesema kwamba kocha huyo mwenye umri wa miaka 62 alimtaka katika timu yake mpya, Old Trafford.
"Baada ya mechi aliniomba nije Manchester," Robben alisema akihojiwa na kituo cha Televisheni cha Uholanzi, NOS.
Amekosekana: Louis van Gaal amemkosa Arjen Robben aliyetaka kuhamia nays Manchester United
Lakini kwa bahati mbaya kwa mashabiki wa United, Robben amepiga chini ombi hilo na kusema: "Nina furaha sana kwa mahali nilipo. Nilimuambia (Van Gaal) hivyo. Van Gaal ni kocha bora niliyewahi kuwa naye. Tumekuwa a uhusiano mzuri sana, lakini siwezi kuhama. Niko sehemu sahihi Bayern, hivyo sina cha kufanya na Van Gaal au United,".
Baadaye na Van Gaal akathibitisha nia yake ya kumsajili Robben atue Old Trafford. "Wakati wowote anakaribishwa. Lakini anajua hiki yeye mwenyewe,"amesema.
Twende Old Trafford: Van Gaal ameshindwa kumshawishi Robben ahamie Old Trafford