MZEE WA KUNG'ATANG'ATA LUIS SUAREZ HUYOO BARCELONA

No Comments
article-2677164-1F43D0D600000578-630_634x347
Anaondoka? Liverpool na Barcelona wanatarajia kuanza mazungumzo juu ya kuuziana Luis Suarez.
KLABU za Liverpool na Barcelona zinatarajia kuanza kufanya mazungumzo juu ya bei ya awali ya paundi milioni 80 ili kuuziana mshambuliaji mweye matatizo kwa sasa, Muurguay, Luis Suarez.
Mtandao wa michezo wa Sportsmail unafahamu kuwa maofisa wa Liverpool, akiwemo mkurugenzi mtendaji, Ian Ayre, wamekubali kukutana na mkurugenzi wa michezo wa FC Barcelona, Raul Sanllehi,  mjini London ili kujadiliana thamani ya mchezaji huyo mwenye miaka 27.
Barcelona wanatazamiwa kutoa paundi milioni 60 kwa kuzingatia kuwa Suarez amefungiwa miezi minne kucheza soka baada ya kumng`ata beki wa Italia, Giorgio Chiellini.
Liverpool hawapo tayari kushusha bei ya Suarez, lakini wanataka kumhusisha mshambuliaji wa Barcelona Alexis Sanchez kama sehemu ya makubaliano hayo.
Controversial: Suarez has been linked with a move to Barcelona after being banned from football for four months
Suarez anahusishwa kujiunga na Barcelona baada ya kufungiwa miezi minne kucheza soka.
Barcelona wanasema mchezaji wao wa kimataifa wa Chile ana thamani ya paundi milioni 35, lakini tayari wameshakataa ofa ya paundi milioni 20 kutoka kwa Juventus ya Italia iliyokuwa na nia ya kumsajili nyota huyo mwenye miaka 25.
- See more at: http://shaffihdauda.com/?p=2969#sthash.oxTLgBpp.dpuf

Dear readers, after reading the Content please ask for advice and to provide constructive feedback Please Write Relevant Comment with Polite Language.Your comments inspired me to continue blogging. Your opinion much more valuable to me. Thank you.