LOGARUSIC AELEZEA ANAVYOTAKA KUSHANGILIA USHINDI WA SIMBA

No Comments

Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic amesema anataka kuwa na furaha na hakuna kitakachomfurahisha zaidi ya kuona kikosi chake kinashinda.

Loga raia wa Croatia amesema anataka kuwa na maandalizi ya uhakika katika kipindi cha sasa kwa kuwa ndiyo muhimu kumpatia ushindi.
“Ukikosea katika kipindi cha mwanzo, basi ujue una kazi ngumu. Furaha ya kufanya vizuri ni jambo jema kwa kocha yoyote.
“Natamani kushangilia kila wakati, lakini najua furaha itapatikana kama nitafanya mambo ya uhakika sasa na wachezaji wanapaswa kujituma na kunivumilia,” alisema Logarusic.
Tayari Loga ametua jijini Dar es Salaam na anaanza kazi kesho kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kujiandaa na msimu mpya wa 2014-15.

Dear readers, after reading the Content please ask for advice and to provide constructive feedback Please Write Relevant Comment with Polite Language.Your comments inspired me to continue blogging. Your opinion much more valuable to me. Thank you.