PSG YATAKA KUIPOKONYA TONGE MDOMOMI MAN UNITED, DI MARIA HUENDA AKATUA UFARANSA

No Comments
KLABU ya Paris Saint-Germain ipo kwenye nafasi nzuri zaidi ya kumpata winga wa Real Madrid, Angel Di Maria, ambaye pia anatakiwa na Manchester United. 
Mshambuliaji huyo wa pembeni wa Argentina mustakabali wake haueleweki Bernabeu baada ya Real kuwa katika mpango wa kumsajili nyota wa Colombia, James Rodriguez. 
Pamoja na hayo, kocha Carlo Ancelotti hayuko tayari kumpoteza Di Maria, ambaye alikuwa na mchango mkubwa msimu uliopita wakati Real ikitwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, ingawa Rais Florentino Perez amemtambulisha Rodriguez kama 'galactic mpya'.
Yuko juu: Di Maria alikuwa ana msimu mzuri uliopita Real Madrid na sasa yuko njiani kuondoka

PSG sasa wanaamini wanaongoza mbio za kuwania saini ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, Di Maria, ambaye ana miaka minne katika Mkataba wake ya kuwa kazini Madrid. 
Real inaweza kusikiliza ofa ya kuanzia Pauni Milioni 50 kumuuza Di Maria owe kutoka kutoka PSG na United.

Dear readers, after reading the Content please ask for advice and to provide constructive feedback Please Write Relevant Comment with Polite Language.Your comments inspired me to continue blogging. Your opinion much more valuable to me. Thank you.