HABARI MBAYA KWA WAFARANSA KOMBE LA DUNIA

No Comments
Ribery nje ya Kombe la Dunia
Mkufunzi wa Ufaransa amedhibitisha kuwa mshambulizi Frank Ribery hatashiriki kombe la dunia kutokana na jeraha.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 na anayechezea klabu ya Bayern Munich alijeruhiwa mgongoni wakati wa mazoezi siku ya Ijumaa.

‘’Hataweza kufanya mazoezi wala kucheza kwa majuma kadhaa.”“Ilimbidi kuwacha kufanya mazoezi kwa kuwa alikuwa akihisi uchungu mwingi sana,” Deschamps aliwaambia wanahabari baadaye.

Ribery amejeruhi mgongo mazoezini
Lyon's Clement Grenier pia atakosa mashindano hayo kwa jeraha la nyonga.
Kiungo cha kati wa Southampton Morgan Schneiderlin na mshambulizi wa Montpellier Remy Cabella wamejumuishwa kikosini ili kucheza kwa niaba ya wawili hao.
Ribery alipelekwa kupigwa picha ya MRI, ambayo ilidhibitisha kiwango cha jeraha hilo.

Riberi alichaguliwa kuwa mchezaji wa tatu bora zaidi duniani mwaka wa 2013 nyuma ya mshindi wa Ballon d’Or Christiano Ronaldo wa Real Madrid na mshambulizi wa Barcelona Lionel Messi.

Dear readers, after reading the Content please ask for advice and to provide constructive feedback Please Write Relevant Comment with Polite Language.Your comments inspired me to continue blogging. Your opinion much more valuable to me. Thank you.