DUH! HII YAWEZA KUWA MBAYA KWA WAMBURA

No Comments
BAKHRESA (KULIA), KUSHOTO KWAKE NI KAMGUNA, MMOJA WA WAJUMBE WA KAMATI YA UCHAGUZI YA SIMBA.

Mjumbe wa kamati ya uchaguzi ya Simba, Amin Bakhresa ameibuka na kumtaka Michael Richard Wambura, kutoa ushahidi kuhusiana na kashfa ya  rushwa na rushwa ya ngono.
Bakhresa ambaye ni mmoja wa viongozi wakongwe wa soka nchini, amesema kamati kwa ujumla imekerwa na maneno ya Wambura aliyeenguliwa.
“Hivyo tunataka atoe ushahidi, sisi tuko tayari na kamati hii ina watu waadilifu sana, sasa kauli za kubahatisha za Wambura si nzuri.
“Kama unakumbukam kamati hii ndiyo ilimpitisha Wambura kugombea uchaguzi Simba kwa kuwa waliompinga hawakuwa na vielelezo.
“Kamati ya rufaa ya TFF ikamkata, nashangaa wakati huo hakusema alitoa rushwa kupita.
“Sasa leo amekatwa baada ya waliokata rufaa kuwa na vielelezo sahihi, ajabu anatutukana tena maneno makali sana.
“Hivyo akanushe au alete ushahidi, la sivyo tutaenda mbele zaidi na kulifikisha sehemua ambayo suala hili litashughulikiwa,” alisema Bakhresa.
Wambura alilaumu kwamba kuna rushwa inatembea kwa lengo la kummaliza na kusema pia kuna rushwa ya ngono.
Wambura alienguliwa baada ya kuonekana uanachama wake Simba ulisimamishwa baada ya yeye kwenda mahakamani kuishitahi klabu hiyo mwaka 2010.
Tayari Wambura ambaye kundi lake limekuwa lile linalofanya vurugu lukuki ingawa wengi wao wamebainika si wanachama Simba, ameishakata rufaa TFF.
http://salehjembe.blogspot.com/

Dear readers, after reading the Content please ask for advice and to provide constructive feedback Please Write Relevant Comment with Polite Language.Your comments inspired me to continue blogging. Your opinion much more valuable to me. Thank you.