NDUMBALO AMCHANA WAMBURA

No Comments


Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Dokta Damas Daniel Ndumbaro amefichua siri na kusema yeye ni mwalimu wa Michael Richard Wambura.

Ndumbaro amesema Wambura ni mwafunzi wa sheria mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu Huria jijini Dar es Salaam ambako yeye ni mwalimu.
“Sasa hapa nani atamfundisha mwenzake sheria, mimi ni mwalimu naye ni mwanafunzi. Mimi ndiye ninayeweza kumfundisha yeye.

“Najua uwezo wa Wambura darasani, lakini suala la kimaadili tu ndiyo linazuia kusema kwenye vyombo vya habari.
“Wambura anasema ananipa nafasi ya kwenda kusoma, lakini nashangazwa na hilo, mimi ni dokta nina PhD. Hilo ndilo darasa la mwisho duniani.

“Kama ni uprofesa, basi sitawiki kukaa darasani, hivyo yeye ndiye anapaswa kusoma.
“Nimesikia anasumbuka ada, basi hana haja ya kunilipia mimi na badala yake apambane kujiendeleza yeye ambaye bado yuko shule,” alisema Ndumbaro.

Wambura alihoji PhD ya Ndumbaro akidai alifanya mambo kwa kubabaisha hadi kufikia kumsimamisha.
Lakini leo, Ndumbaro amesema asingeweza kujibu suala hilo lakini kwa kuwa Wambura aliishambulia kamati na yeye binafsi, hivyo wameamua kujibu.

“Mimi nilifikiri Wambura angejibu hoja, kwa kuwa yeye alitakiwa kukata rufaa bila ya kuitukana kamati.
“Kwa mtu mwenye akili timamu, asingefanya hivyo, badala yake angekata rufaa na kuwasilisha hoja zake. Hapa tuna barua zake anakili kuondolewa uanachama.
“Lakini yeye amesimamishwa uanachama wake, anaomba kurejeshwa. Sasa anakataa vipi,” alisema Ndumbaro ambaye ni mwanasheria na wakili maarufu nchini.
http://salehjembe.blogspot.com/

Dear readers, after reading the Content please ask for advice and to provide constructive feedback Please Write Relevant Comment with Polite Language.Your comments inspired me to continue blogging. Your opinion much more valuable to me. Thank you.