HABARI MBAYA KWA WAFARANSA KOMBE LA DUNIA

No Comments
Ribery nje ya Kombe la Dunia
Mkufunzi wa Ufaransa amedhibitisha kuwa mshambulizi Frank Ribery hatashiriki kombe la dunia kutokana na jeraha.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 na anayechezea klabu ya Bayern Munich alijeruhiwa mgongoni wakati wa mazoezi siku ya Ijumaa.

‘’Hataweza kufanya mazoezi wala kucheza kwa majuma kadhaa.”“Ilimbidi kuwacha kufanya mazoezi kwa kuwa alikuwa akihisi uchungu mwingi sana,” Deschamps aliwaambia wanahabari baadaye.

Ribery amejeruhi mgongo mazoezini
Lyon's Clement Grenier pia atakosa mashindano hayo kwa jeraha la nyonga.
Kiungo cha kati wa Southampton Morgan Schneiderlin na mshambulizi wa Montpellier Remy Cabella wamejumuishwa kikosini ili kucheza kwa niaba ya wawili hao.
Ribery alipelekwa kupigwa picha ya MRI, ambayo ilidhibitisha kiwango cha jeraha hilo.

Riberi alichaguliwa kuwa mchezaji wa tatu bora zaidi duniani mwaka wa 2013 nyuma ya mshindi wa Ballon d’Or Christiano Ronaldo wa Real Madrid na mshambulizi wa Barcelona Lionel Messi.
SAKATA LA WAMBURA SIMBA LAIBUKIA FIFA

SAKATA LA WAMBURA SIMBA LAIBUKIA FIFA

No Comments
20131102-114737.jpg

Wanachama Simba waenda FIFA….

By Israel Saria on June 5, 2014
Wasema Malinzi anambeba Wambura!
WANACHAMA watano wa Simba wametuma barua katika Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) wakimshtaki, Rais wa Shirikisho la Mchezo huo Nchini (TFF), Jamal Malinzi, wakidai ‘anampendelea’ aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Rais katika Uchaguzi Mkuu wa Simba, Michael Wambura.
Kamati ya Uchaguzi ya Simba ilimuengua Wambura katika mchakato wa uchaguzi kutokana na mgombea huyo kusimamishwa uanachama tangu Mei 5 mwaka 2010 kufuatia kufungua kesi kwenye Mahakama ya Kisutu yenye namba 100/2010 akiushitaki uongozi uliokuwa madarakani wakati huo.
Wanachama hao watano wa Simba waliowasilisha malalamiko yao FIFA dhidi ya Malinzi ni pamoja na  Masoud Hassan mwenye kadi namba 0500, Salehe Shahame (05596), Frank Pastoli (01288), Rajab Mtitu (01146) na Ally Mkumba (02519).
“Wambura ana kesi ya kimaadili na Kamati za Uchaguzi hazina mamlaka ya kuziamua kwa sababu kupeleka masuala ya soka kwenye mahakama za kawaida ni kosa kama katiba ya FIFA inavyoeleza,” ilisema sehemu ya barua hiyo.
Wanachama hao wa wadai katika barua hiyo iliyoandikwa Juni 3 mwaka huu kuwa Malinzi anadaiwa kuishinikiza Kamati ya Rufaa na Kamati ya Maadili kumrejesha Wambura kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi licha ya kufanya kosa hilo linaloenda kinyume na katiba ya Simba, TFF na FIFA.
Katika barua yao wameeleza kwamba tayari Malinzi ameshatoa maelekezo kwa kamati ya Rufaa imrejeshe mgombea huyo kwenye uchaguzi huo.
Katika barua hiyo wanachama hao wametuma nakala kwa viongozi wanaoshughulika na masuala ya uanachama ambao ni Thiery Reganass, Primo Corvaro na Ashford Mamelodi.
Malinzi aliliambia gazeti hili jana kwamba yeye na TFF haina nia ya kuingilia mchakato wa uchaguzi wa Simba ambao unatarajia kufanyika Juni 29 mwaka huu.
Kiongozi huyo wa juu alisema kwamba shirikisho hilo inachofanya ni kuhakikisha katiba na kanuni za uchaguzi kwa wanachama wake zinafuatwa.
Tayari kamati ya Rufaa ya Uchaguzi imesema kuwa itasikiliza rufaa ya Wambura Jumatatu Juni 9.
TANZANIASPORT
MBEYA CITY MWENDO MDONDO YALAMBA MKATABA WA MILIONI 360

MBEYA CITY MWENDO MDONDO YALAMBA MKATABA WA MILIONI 360

No Comments
Kampuni ya Bin Slum Tyre Company Limited leo imeingia mkataba rasmi wa kuidhamini timu ya soka ya Mbeya City Council ya jijini Mbeya katika hafla fupi ya utiaji saini mkataba huo iliyofanyika katika ukumbi wa ofisi za jiji la Mbeya, Mkataba huu utakuwa wa miaka miwili, ambao utawafanya Mbeya City kunufaika na kiasi hicho cha fedha kwa muda huo wote wa mkataba.
Binslum 2Binslum 8Mkataba huo wenye thamani ya milioni 360 ambao kampuni hiyo itakuwa ikitangaza bidhaa za RB Battery katika jezi za timu ya Mbeya city, na pia chini ya namba nyuma ya jezi itaandikwa kampuni ya Bin Slum Tyre Company.
Binslum 4Akiongea wakati wa utiaji saini wa mkataba huo jijini Mbeya, Mkurugenzi wa , Binslum Tyre Mohamed Binslum, alisema “Tumefikia makubaliano haya baada ya kuona uongozi wa timu ya Mbeya City umejipanga vizuri katika kuendesha timu yao, na kupata mwitikio mkubwa kutoka kwa wananchi wa Jiji la Mbeya pamoja na mikoa ya Kanda ya Kusini, hivyo itakuwa ni fursa nzuri kwa kuzitangaza betri zetu za RB ambazo pia Mbeya ni soko letu kubwa”.” Kampuni yetu ina bidhaa nyingi kama vile aina nzuri ya matairi ya Double Star na Vee Rubber”. Aliongeza Binslum.
IMG_20140605_120725Meya wa jiji la Mbeya Mheshimiwa Athanas Kapunga, ameishukuru kampuni ya Binslum kwa kukubali kuingia mkataba huo ambao utaisaidia timu kuongeza ufanisi wa kuindesha timu yao. “Napenda kuishukuru mkurugenzi wa Binslum Tyre Company Limited kupitia betri za RB kwa kuonyesha nia ya dhati katika kuedeleza soka la jiji la Mbeya na Tanzaniam kwa ujumla, nina imani msimu ujao tutakuwa na uwezo na kasi kubwa sana kama vile taa za gari zinavyotoa mwanga wa taa mkali zikiwa na betri za RB”. Alisema Meya wa jiji la Mbeya.
IMG_20140605_122200Naye Meneja masoko na uhusioano wa jamii wa kampuni ya Binslum Tyre Bw. Peter Ngassa alisema “Binslum Tyre Company tumeamua kuwekeza katika mpira wa miguu Tanzania kwa sababu kuna nafasi nzuri ya kutangaza bidhaa zetu kupitia eneo hilo na kutoa matokeo chanya pia kwa Mbeya City kutimiza ndoto zao”. Pia kupitia betri imara za RB tunaitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete anaoutoa kila mara akiagiza makampuni mbalimbali kujitokeza kudhamini michezo kwa njia mbalimbali.
SHAFFIHDAUDA

STARS KUWASILI LEO, PONGEZI ZAMIMINIKA

No Comments

Kikosi cha Taifa Stars ambacho jana (Juni 1 mwaka huu) kiliitupa Zimbabwe (Mighty Warriors) nje ya michuano ya Afrika baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 kinarejea nchini leo (Juni 2 mwaka huu) kutoka Harare.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam saa 12.30 jioni kwa ndege ya Kenya Airways ikitokea Harare kupitia Nairobi.

Stars imefuzu kucheza raundi inayofuata kwa ushindi wa jumla ya mabao 3-2, kwani awali (Mei 18 mwaka huu) iliifunga Zimbabwe bao 1-0 katika mechi ya kwanza iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katika raundi ya pili, Taifa Stars itacheza na Msumbiji ambapo itaanzia nyumbani kati ya Julai 19 na 20 mwaka huu, wakati mechi ya marudiano itafanyika Msumbiji kati ya Agosti 2 na 3 mwaka huu.

Wakati huo huo, Taifa Stars imeendelea kupokea salamu za pongezi kutoka kwa wadau mbalimbali baada ya kufanikiwa kuvuka kikwazo hicho cha kwanza katika harakati zake za kucheza Fainali za Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.

Salamu hizo zimetoka kwa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya (MREFA), Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Manyara (MARFA), mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) akiwakilisha Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA), John Kadutu, na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Ahmed Idd Mgoyi.
SALEHJEMBE
BAADA KUTEMWA MAN U MOYES SASA AFUNGUKA

BAADA KUTEMWA MAN U MOYES SASA AFUNGUKA

No Comments
20140601-205709-75429461.jpg

Moyes: Laiti ningepewa muda Man United

By Israel Saria on June 1, 2014
*Asema kuna ofa nyingi lakini anapumzika
Kocha wa zamani wa Manchester United, David Moyes anaamini alistahili kupewa muda zaidi kuwanoa Mashetani Wekundu hao.
Moyes (51) aliyefukuzwa kazi akiwa mwezi wa 10 katika mkataba wake wa miaka mitano, anasema Man U haiwezi kurekebishwa haraka, bali inahitaji muda.
Anasema ni bahati mbaya kwamba hakupewa muda huo, kwamba amejifunza mengi katika muda huo na kwamba aliyemsaidia tu ni Mskochi mwenzake, Sir Alex Ferguson aliyempendekeza kuvaa viatu vyake baada ya kukaa hapo kwa miaka 26.
Moyes anasema amepata ofa nzuri kutoka kwa klabu moja au zaidi lakini anafikiria kupumzika nje ya soka kwa muda badala ya kuzikubali.
Inaelezwa kwamba Celtic, mabingwa wa Scotland wameshamfuata kutaka azibe pengo la Mskochi mwenzake, Neil Lennon.
“Naamini nitakuwa na busara zaidi na kocha mwenye ujuzi zaidi baada ya kuwa kocha pale Old Trafford,” anasema Moyes ambaye nafasi yake inachukuliwa na Mdachi Lous van Gaal.
Moyes anasema kwamba angepewa muda angetekeleza vyema mpango wake wa muda mrefu wa kuifufua United na kwamba baada ya kuondoka alitumiwa ujumbe wa kumtakia heri na wachezaji, wakiwamo Wayne Rooney na Darren Fletcher.
Anasema Fergie alimshauri baadhi ya maeneo ya kurekebisha na kufanyia mabadiliko, mipango aliyokuwa ameshaianza lakini cha kushangaza akafukuzwa kabla hata mchakato haujafika mbali.
Kinachoshangaza katika wakati wake huo wa miezi 10 ni Man U kuvunja rekodi kwa kufanya vibaya wakati ni kikosi kile kile kilichokuwa kimetwaa ubingwa msimu uliotangulia chini ya Fergie.
TANZANIASPORT.COM
GHANA KUWATAJA WACHEZAJI WA KOMBE LA DUNIA BRAZIL WAKIONGOZWA NA GYAN

GHANA KUWATAJA WACHEZAJI WA KOMBE LA DUNIA BRAZIL WAKIONGOZWA NA GYAN

No Comments
Ghana announce final World Cup squad
 
KOCHA mkuu wa timu ya taifa ya Ghana, Kwesi Appiah ametaja kikosi chake cha mwisho cha wachezaji 23 kwa ajili ya fainali za kombe la dunia zinazoanza kushika kasi mwezi huu nchini Brazil.
Kikosi hicho cha Appiah kinajumuisha wachezaji 16 wanaokwenda kucheza fainali hizo kwa mara ya kwanza, huku nahodha Asamoah Gyan na Sulley Muntari wakiwa wakongwe wanaokwenda kucheza fainali zao za tatu mfululizo, wakati Jonathan Mensah, Michael Essien,  Kwadwo Asamoah, Andre Ayew na  Kevin-Prince Boateng wanakwenda kucheza fainali hizo kwa mara ya pili.
Kocha huyo mwenye miaka 53 amewaacha majeruhi Jerry Akaminko, Jeffrey Schlupp na David Accam  katika kikosi hicho kinachoelekea Miami kuweka kambi ya maandalizi ya mwisho ambapo kitacheza mechi ya kirafiki juni 9 dhidi ya Korea kusini
Akaminko alipata majeruhi jana jumamosi katika kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Uholanzi kwenye mechi ya kirafiki na atafanyiwa upasuaji utakaomfanya akae nje ya uwanja kwa miezi mitatu.
Ghana iliyofika robo fainali mwaka 2010 ipo kundi G pamoja na nchi za Marekani, Ujeruman na Ureno.
Kikosi kamili:
Walinda Mlango:Fatau Dauda (Orlando Pirates), Adam Kwarasey (Stromsgodset), Stephen Adams (Aduana Stars)
Mabeki: Samuel Inkoom (Platanias), Daniel Opare (Standard Liege/Porto), Harrison Afful (Esperance), John Boye (Rennes), Jonathan Mensah (Evian), Rashid Sumalia (Mamelodi Sundowns)
Viungo: Michael Essien (AC Milan), Sulley Muntari (AC Milan), Rabiu Mohammed (Kuban Krasnodar), Kwadwo Asamoah (Juventus), Emmanuel Agyemang-Badu (Udinese), Afriyie Acquah (Parma), Christian Atsu (Vitesse), Albert Adomah (Middlesbrough), Andre Ayew (Marseille), Mubarak Wakaso (Rubin Kazan)

Washambuliaji: Asamoah Gyan (Al Ain), Kevin-Prince Boateng (Schalke 04), Abdul Majeed Waris (Valenciennes), Jordan Ayew (Sochaux)

MAXIMO ANUKIA YANGA

MAXIMO ANUKIA YANGA

No Comments
1908319_739353366128611_8170079415409113241_n 
Mkutano Mkuu wa marekebisho ya baadhi ya vipengele kwenye Katiba ya Yanga umefanyika na kumalizika salama na furaha kwenye Ukumbi wa Bwalo la Polisi -Oysterbay huku wanachama wakipitisha kipengele cha kuundwa kwa kamati ya maadili.
Mwenyekiti wa klabu ya Yanga SC Yusuf Manji amewaongoza wanachama hai wapatao 1,560 kupitisha kipengele hicho kipya kwa ajili ya maslahi na faida ya Wana Yanga kwani bila kufanya hivyo timu isingeweza kuruhusiwa kushiriki Ligi Kuu msimu ujao.
Aidha katika mkutano huo Manji amewatoa hofu wanachama kwa kuwaambia kuwa usajili unaendelea kufanyika na nafasi zilizobakia ni nne tu hivyo pindi utakapokamilika basi wataweka wazi kila kitu.
Kuhusu nafasi ya Kocha Mkuu Manji amesema Kamati ya Mashindano imemkabidhi mapendekezo yao na kwa sasa yupo kwenye mazungumzo na Marcio Maximo aliyewahi kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa Tanzania kuja kukinoa kikosi cha Jangwani.
Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini Mama Fatma Karume aliongoza kikao cha waachama kilichomuomba Bw Manji kuendelea na uongozi ambapo mwenyeikti alitoka nje na kamati yake ya utendaji na pindi waliporejea walikubali ombi hilo na kusema watafuata taratibu za kikatiba.

Mwisho kupitia mkutano mkuu wa leo wa wanachama umeazimia kuwaongezea muda wa mwaka mmoja Mwenyekiti Yusuf Manji pamoja na Makamu wake Clement Sanga ili waweze kukamilisha masuala ya katiba na kuweza kuandaa mkutano wa uchaguzi baada ya katiba kupitishwa na TFF.

DUH! HII YAWEZA KUWA MBAYA KWA WAMBURA

No Comments
BAKHRESA (KULIA), KUSHOTO KWAKE NI KAMGUNA, MMOJA WA WAJUMBE WA KAMATI YA UCHAGUZI YA SIMBA.

Mjumbe wa kamati ya uchaguzi ya Simba, Amin Bakhresa ameibuka na kumtaka Michael Richard Wambura, kutoa ushahidi kuhusiana na kashfa ya  rushwa na rushwa ya ngono.
Bakhresa ambaye ni mmoja wa viongozi wakongwe wa soka nchini, amesema kamati kwa ujumla imekerwa na maneno ya Wambura aliyeenguliwa.
“Hivyo tunataka atoe ushahidi, sisi tuko tayari na kamati hii ina watu waadilifu sana, sasa kauli za kubahatisha za Wambura si nzuri.
“Kama unakumbukam kamati hii ndiyo ilimpitisha Wambura kugombea uchaguzi Simba kwa kuwa waliompinga hawakuwa na vielelezo.
“Kamati ya rufaa ya TFF ikamkata, nashangaa wakati huo hakusema alitoa rushwa kupita.
“Sasa leo amekatwa baada ya waliokata rufaa kuwa na vielelezo sahihi, ajabu anatutukana tena maneno makali sana.
“Hivyo akanushe au alete ushahidi, la sivyo tutaenda mbele zaidi na kulifikisha sehemua ambayo suala hili litashughulikiwa,” alisema Bakhresa.
Wambura alilaumu kwamba kuna rushwa inatembea kwa lengo la kummaliza na kusema pia kuna rushwa ya ngono.
Wambura alienguliwa baada ya kuonekana uanachama wake Simba ulisimamishwa baada ya yeye kwenda mahakamani kuishitahi klabu hiyo mwaka 2010.
Tayari Wambura ambaye kundi lake limekuwa lile linalofanya vurugu lukuki ingawa wengi wao wamebainika si wanachama Simba, ameishakata rufaa TFF.
http://salehjembe.blogspot.com/

FOOTBALL

ATHLETIC