HANS POPPE, WAMBURA MOTO WAWAKA UCHAGUZI SIMBA SC, NDUMBARO KUANIKA HATIMA YA MAPINGAMIZI KESHO

No Comments

wambura

Richard Wambura sasa `vitani` na Zacharia Hans Poppe
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
MWENYEKITI wa kamati ya uchaguzi ya Simba unaotarajia kufanyika juni 29 mwaka huu, mwanasheria na wakala wa wachezaji wa FIFA, Dkt. Damas Daniel Ndumbaro anatarajia kuanika hatima ya majina ya wagombea wote waliowekewa pingamizi.
Wana Simba wengi wanasubiri kwa hamu kusikia hatima ya wagombea wa nafasi mbalimbali waliowekwa kitanzini na baadhi ya wanachama wa klabu hiyo kwasababu tofauti tofauti.
Mgombea Urais, Michael Richard Wambura ni moja ya wagombea wa Urais aliyewekewa pingamizi, hivyo wafuasi wake waliomsindikiza kwa mbwembwe nyingi wakati wa kuchua na kurudisha fomu wanasubiri kwa hamu hatima yake.
Kamati ya uchaguzi jana imefanya kazi ya kuwasikiliza watu walioweka mapingamizi na wagombea waliowekewa pingamizi.
Awali Ndumbaro alisema kamati yake haitamuengua mgombea yeyote isipokuwa kanuni za uchaguzi za TFF na katiba ya Simba ndio itamuengua mgombea.
Ndumbaro alisema kamati yake itawaondoa wale wote walioenda kinyume na kanuni za uchaguzi na kusisitiza kuwa kamati yake ina watu makini na haitathubutu kupindisha sheria.
hans-poppeHans Poppe hamtaki Wambura katika nafasi ya urais, chaguo lake ni Aveva.
Wakati hayo yakijiri, Richard Wambura amewasilisha malalamiko yake kwa kamati ya uchaguzi akisema baadhi ya watu wamekiuka kanuni za uchaguzi kwa kuwapigia kampeni baadhi ya wagombea kabla ya muda uliotajwa.
“Nimepata ushahidi wa CD ya Hans Poppe akiwaombea kura Aveva na Kaburu. Pia amasema mimi niliwahi kuiba hela Simba. Nimekabidhi CD kwa Ndumbaro kwa hatua zaidi na aeleze niliiba wapi hela hizo”. Alisema Wambura, moja ya wagombe wa Urais.
“Pia nitapeleka CD katika kamati ya maadili ya TFF. Mtu hawezi kutukana bila sababu”.
“Poppe anasema wasipochaguliwa Kaburu na Aveva ataacha kuisaidia Simba. Anasema ataondoka katika uongozi. Hii ni nini sasa kama sio kwenda kinyume na taratibu”.Alikaririwa Wambura.
Mwishoni mwa wiki, mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba sc, Keptein Zacharia Hans Poppe alizungumza na mtandao huu na kuweka wazi msimamo wake kuwa endapo Aveva na kaburu hawatachaguliwa katika uchaguzi wa Juni 29 atabwaga manyanga.
Poppe alisema amechoka kutoa fedha zake bila mafanikio yoyote, hivyo anahitaji timu ya uongozi ya Aveva na Kaburu kwani wanaweza kufanya kazi vizuri.
Mwanajeshi huyo wa zamani wa JTWTZ alibainisha kuwa Wambura hana uwezo wa kuiongoza Simba kwani wakati wake wa uongozi hakuna alichokifanya.
Pia alimponda Jamhuri Kiwhelo `Julio` kuwa hajawahi kufanya lolote akiwa Simba kwani yeye alikuwa kocha na alikuwa analipwa mshahara, wakati Kaburu aliyejitahidi kusuka Simba B wakati wa uongozi wake na kuzalisha wachezaji mahiri wakiwemo Ramadhan Singamo `Messi`, Harun Chanongo, Said Ndemla na wengineo, hivyo anafaa kuwa makamu wa rais.

Dear readers, after reading the Content please ask for advice and to provide constructive feedback Please Write Relevant Comment with Polite Language.Your comments inspired me to continue blogging. Your opinion much more valuable to me. Thank you.