TP MAZEMBE YAMSAJILI ALI SADIKI

TP MAZEMBE YAMSAJILI ALI SADIKI

No Comments
Rais wa klabu ya TP Mazembe Moise Katumbi
Klabu bingwa ya soka katika Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo, TP Mazembe, imemsajili mchezji wa kimaataifa raia wa Zimbabwe, Ali Sadiki.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, amepewa mkataba wa miaka mitano, kwa kupendeza kwa mchezo wake wakati wa wiki moja la majaribio kutoka katika klabu ya Stars ya Zimbabwe.

"Mazembe ni klabu kubwa na tunataka wachezaji wazuri zadi kutoka kote duniani kuja hapa,’’ alisema Katumbi.Kusainiwa kwa Sadiki ni sehemu ya meneja wa klabu ya TP Mazembe, Moise Katumbi kuimarisha klabu hiyo katika ligi ya taifa.

Ikiwa kuna wachezaji wazuri zaidi, hata barani Ulaya wanakaribishwa kuja hapa.’’
Mazembe ni washindi mara nne wa ligi ya klabu bingwa Afrika na sasa wako katika robo fainali ya ligi ya mwaka huu sawa na AS Vita, Zamalek ya Misri, na Al-Hilal ya Sudan.
Sadiki alikuwa katika timu ya taifa ya Zimbabwe ambayo mwaka huu ilifika nusu fainali ya mabingwa wa Afrika.
Wakati huohuo, mchezaji wa Zambia Nathan Sinkala anayesakata kabumbu ya kimataifa, atamaliza msimu wake na klabu ya Sochaux ya Ufaransa mwaka huu

Katumbi amesema kuwa kuna vilabu kadhaa viavyomtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 ifikapo Januari mwaka ujao. 
MECHI YA TAIFA STARS NA ZIMBABWE KUONESHWA NA AZAM TV

MECHI YA TAIFA STARS NA ZIMBABWE KUONESHWA NA AZAM TV

No Comments
HUZUNI! MBEYA CITY FC YACHAPWA 1-0 NA VICTORIA UNIVERSITY ROBO FAINALI

HUZUNI! MBEYA CITY FC YACHAPWA 1-0 NA VICTORIA UNIVERSITY ROBO FAINALI

No Comments
DSCF5413Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya CECAFA Nile Basin Cup, Mbeya City fc wameaga mashindano hayo baada ya kufungwa bao 1-0 dhidi ya Victoria University ya Uganda katika mchezo wa robo fainali uliomalizika dakika chache zilizopita mjini Khartoum.
Mbeya City wametolewa katika michuano hiyo wakiwa wameshinda mechi moja, kufungwa moja na kutoka suluhu mechi moja katika hatua ya makundi.
Lakini wamepoteza mechi ya pili katika mashindano haya baada ya kufungwa hatua ya robo fainali na kufungashiwa virago.
Afisa habari wa Mbeya City fc, Freddy Jackson amesema wanashukuru kwa kilichotokea kwani ndio matokeo ya mpira wa miguu.
Freddy amesema wachezaji wamejitahidi kucheza kwa juhudi, lakini hawakuwa na bahati.
“Ndugu tunashukuru kwa maombi yenu, alichotupangia mungu ndicho tulichopata. Mechi imemalizika , Mbeya city O victoria 1, hivyo basi tumeyaaga mashindano”. Amesema Freddy.
SHAFFI DAUDA.COM
UGANDA RWANDA KENYA ZASONGA MBELE KAZI KWA TAIFA STARS

UGANDA RWANDA KENYA ZASONGA MBELE KAZI KWA TAIFA STARS

No Comments

BAO PEKEE LA MASSA LAWAVUSHA UGANDA HATUA INAYOFUATA, RWANDA YAIKANYAGA LIBYA 3-0

Football - 2014 Fifa World Cup Qualifier - Uganda Vs Angola - Mandela Stadium - Namboole - KampalaNa Baraka Mpenja, Dar es salaam
UGANDA The Cranes imefanikiwa kusonga hatua inayofuata katika michuano ya kuwania kupangwa hatua ya makundi kusaka tiketi ya kucheza fainali za kombe la mataifa ya Afrika, AFCON 2015 nchini Morocco baada ya kufanikiwa kuiondosha Madagascar kwa wastani wa mabao 2-2, lakini Uganda wamenufaika kwa faida ya bao la ugenini.
Uganda jioni hii wameibuka na ushindi wa bao 1-0 mjini Kampala katika mchezo wa marudiano, na mechi ya kwanza walilala kwa mabao 2-1 nchini Madagascar.
Bao pekee la Uganda limefungwa na Geoffrey Massa katika dakika ya 12 ya kipindi cha kwanza na kuwasimamisha vitini mashabiki waliofurika kuitazama timu yao.
Katika mchezo mwingine uliomalizika jioni hii, timu ya taifa ya Rwanda “Amavubi` imefanikiwa kusonga mbele kwa wastani wa mabao 3-0 kutokana na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Libya walioupata jioni hii.
Mabao yote ya Rwanda yamefungwa na Dady Birori katika dakika ya 39`, 64 na 72.
Mechi ya kwanza Rwanda walitoka suluhu ya bila kufungana na Libya mjini Tripoli.
Mechi nyingine zinazopigwa leo ni baina ya Guines Bissau dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya kati, wakati nao Sierra Leone watachuana na Swaziland.
Mechi baina ya Seychelles dhidi ya Gambia imeahirishwa.
SHAFFIDAUDA.COM
CHRISTIANO RONALD 100% KOMBE LA DUNIA

CHRISTIANO RONALD 100% KOMBE LA DUNIA

No Comments
Screen Shot 2014-05-30 at 12.09.53 PM
Hili ndio gari alilowasili nalo.
Ni jana tu May 29 2014 Cristiano Ronaldo ametajwa kushika namba moja kwenye list ya mastaa kumi wa soka ambao wanavutia kibiashara na kufanya kazi na makampuni makubwa ya kibiashara duniani.
Hii post inahusu kuwasili kwa Ronaldo kwenye hoteli timu yake ya taifa ya Portugal ilikoweka makazi ya muda kujiandaa na kombe la dunia litakaloanza siku chache zijazo nchini Brazil.
Screen Shot 2014-05-30 at 12.46.45 PMKulikua na mashabiki wengi waliokua wakimsubiria wakiwemo kina mama, baba na watoto ambao wengine walijaribu hata kumgusa, wengine kumsemesha na wengine kumpiga picha.
Screen Shot 2014-05-30 at 12.46.37 PM
Screen Shot 2014-05-30 at 12.02.32 PM
Screen Shot 2014-05-30 at 12.46.22 PM
Yaani huyu mtoto hakuamini kamshika Ronaldo…. hahahha hii picha ya huyu mtoto nimeipenda.

REAL MADRID YAADHIBIWA KWA UBAGUZI WA RANGI

REAL MADRID YAADHIBIWA KWA UBAGUZI WA RANGI

No Comments

Shirika la kandanda la Europa, UEFA, limeiwekea vikwazo timu ya mpira ya Real Madrid kwa makosa ya mashabiki wao, waliotoa ishara na kejeli za ubaguzi wa rangi wakati wa moja ya mechi zake.

Tukio hilo lilifanyika April wakati wa mechi ya nusu fainali kati ya mabingwa hao wa sasa wa kombe hilo la UEFA, na mahasimu wao,mabingwa wa zamani wa Bayern Munich.

Miongoni na adhabu walizopewa ni kufunga maeneo mawili ya uwanja wao wa Bernabeu wakati wa mechi yao itakayokuja ya UEFA na watapaswa kuweka mabango yaliyo na maandishi 'No to Racism' yaani 'Twakataa ubaguzi wa rangi!.
MBWANA SAMATTA HATIHATI KUIKOSA MECHI ZA TAIFA STARS DHIDI YA ZIMBABWE

MBWANA SAMATTA HATIHATI KUIKOSA MECHI ZA TAIFA STARS DHIDI YA ZIMBABWE

No Comments
10418977_738351759562105_7960579550010362518_nMbwana Samatta siku alipoumia wakati TP Mazembe ikikabiliana na AS Vita mei 25 mwaka huu.
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania anayeichezea klabu ya TP Mazembe ya DR Congo, Mbwana Ally Samatta yuko hatihati kuichezea timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars katika mchezo wa marudiano kesho kutwa (jumapili) dhidi ya Zimbabwe, mjini Harare, kuwania kupangwa hatua ya makundi kusaka tiketi ya kushiriki kombe la mataifa ya Afrika, AFCON mwakani nchini Morocco.
Taarifa za uhakika ni kwamba Samatta alipata majeruhi ya nyama za paja katika mechi ya ligi ya mabingwa barani Afrika mei 25 mwaka huu dhidi ya wapinzani wao AS Vita mjini Lubumbashi, huku akifunga bao pekee katika ushindi wa TP Mazembe wa bao 1-0. Katika mchezo huo, Samatta alitolewa dakika ya 75 kutokana na majeruhi hayo.
Hata hivyo imeelezwa kuwa shirikisho la soka Tanzania, TFF, baada ya kuambiwa na TP Mazembe kuwa Samatta ni majeruhi, wao walilazimisha kumtumia mchezaji huyo.
Ili kukwepa kuonekana msaliti ameamua kusafiri kwenda Zimbabwe pamoja na Thomas Ulimwengu na kuna uwezekano mkubwa kwa Samatta kukaa kama mtazamaji katika mechi hiyo kwani mpaka sasa hajapona majeruhi hayo.
Meneja wa Mbwana Samatta, Jamal Kisongo amethibitisha taarifa za kuumia kwa nyota huyo tegemeo wa TP Mazembe na kueleza kuwa amelazimika kwenda Zimbabwe ili kutoonekana msaliti.
Mahojiano yalikuwa baina ya mwandishi wa mtandao huu na meneja wa Samatta yamekwenda hivi;
Mwandishi: Jamal Kisongo kuna taarifa za Mbwana Samatta kusumbuliwa na majeruhi ya nyama za paja, vipi kuna ukweli wowote?
Kisongo: Ni kweli! Samatta baada ya mechi ya AS Vita na kufunga bao katika dakika ya 62, dakika ya 75 akawa amepata majeraha ya nyama za paja kujivuta, ikabidi pale pale akatishe kuendelea na mechi. Na toka siku hiyo baada ya mechi ile ya Vita mpaka leo hii hajafanya mazoezi, yaani hayuko katika hali vizuri. Mimi nashangaa, leo nikapata taarifa wakati anaenda Zimbabwe. Mtoto mwenyewe kaniambia anakwenda huko, lakini amelazimishwa na ili asionekane msaliti ameamua kwenda.
Mimi binafsi vitu hivi havinivutii sana, kwasababu wakati mwingine Mbwana anacheza vibaya hapa, lakini anakuwa katika hali ngumu. Mara ya mwisho alipata tatizo la kuzomewa hapa, Mbwana hakucheza mechi kwasababu aliumia Zambia. Kwahiyo amekwenda, lakini mechi hii sidhani kama Mbwana atacheza.
Mwandishi: Mbwana amekueleza nini juu ya mawasiliano yake na TFF juu ya hali yake?
Kisongo: Hapana! Yeye ameniandikia `meseji` kuwa anakwenda katika hali hiyo hiyo na yeye hakutaka kuonesha kuwa anakwepa majukumu ya timu ya taifa. Unajua Mbwana si mtu wa maelezo mengi na alivyonitaka ushauri nilimwambia anatakiwa kutii amri ya viongozi wake kwasababu hata mwalimu wa TP Mazembe mwenyewe baada ya kuona hali hiyo akamwambia wewe nenda tu. Na mimi nikamwambia anatakiwa kutii amri ya TFF, labda wanataka aungane na wenzake ili awatie hamasa, labda uwepo wake utachangia kuongeza hamasa, lakini kama atacheza itakuwa ni kumuumiza na itakuwa vibaya.
Hata ripoti ya daktari inaonesha kuwa huyu kijana ni mdogo na hakugongwa, lakini inaoneakana anatumika sana, kwa maana hiyo uchovu ndio unasababisha majeraha haya.
Mwandishi: Samatta anazungumziaje kuzomewa na mashabiki wa Tanzania?
Kisongo: Yeye anasikitika sana kwasababu tukio hilo limetokea mara moja kipindi ambacho alishindwa kuitumika nchi yake baada ya kuumia nchini Zambia ambako TP Mazembe ilikuwa na mechi. Aliumia vibaya kwahiyo alishindwa kuitumikia timu ya taifa. Hata kule Congo hakupata matibabu, alipokuja hapa Tanzania, ilibidi nimshughulikie na kumpeleka Muhimbili. Lakini bahati Mbaya huwa hakuna ufuatiliaji wa watoto hawa kwa TFF.
Mwandishi: Kwanini Samatta anaumia mara kwa mara?
Kisongo: Unajua sasa hivi wachezaji wengi muhimu wameondoka TP Mazembe. Samatta ni jicho la klabu hiyo kwasasa. Umekuwa akitumika sana. Kwa mfano katika mechi na AS Vita, ilijulikana kuwa Samatta ndio siri ya mafanikio ya Mazembe kwa sasa. Alikabwa kwa nguvu na kuumia. Lakini anasikitika sana kushindwa kulitumikia taifa lake. 
Kutokana na majukumu yake, hakuna sababu ya kumchukua kwenye mashindano kama ya `Challenge`. Wanamuongeza mechi nyingi nzito. Wanatakiwa kumuacha apumzike ili anapokuja kwenye mechi kama hizi za kufuzu basi awe katika kiwango kizuri.
Mwandishi: Ipi kauli yako kwa mashabiki wa Tanzania?
Kisongo: Ninachotaka kusema ni kwamba, huyu mtoto analipenda taifa lake, na watanzania wajue hilo na anaumia sana kutolitumikia kwasasa. Hata kama atalazimika kucheza Zimbabwe, tusitarajie makubwa kutoka kwake kutokana na hali halisi ya afya yake.
Mwandishi: Kisongo asante sana na kazi njema.
Kisongo: Shukurani sana nawe pia!
Chanzo: http://shaffihdauda.com/






MAN U WASHANGILIA KIFO CHA GLAZER

MAN U WASHANGILIA KIFO CHA GLAZER

No Comments
20140530-055250-21170371.jpg

Man U washangilia kifo cha Glazer

By Israel Saria on May 30, 2014
Washabiki wa Manchester United wamegawanyika baada ya kutangazwa habari za kifo cha mmiliki wa klabu hiyo, Malcolm Glazer kambi moja ikishangilia waziwazi.
Glazer alisababisha sintofahamu Old Trafford alipoinunua klabu hiyo, ambapo washabiki waliandamana kupinga kuuzwa klabu kwa Mmarekani na pia baadhi ya wachezaji wakajifungamanisha na kambi hiyo.
Washabiki walijitokeza kwenye mitandao ya jamii wakionesha kama vile wametua mzigo fulani kwa kifo chake, licha ya kwamba bado umiliki wa Man U unabaki kwa watoto wake sita ambao wamegawana sawa asilimia 90 ya hisa za klabu na nyingine 10 zimewekezwa kwenye Soko la Mitaji la New York.
“Tuna sherehe kubwa leo kutokana na Glazer kufariki dunia, tutakuwa na karamu ya jelly na ice cream kutokana na kifo hicho,” ni maneno ya kawaida kwenye korido za Old Trafford kwa washabiki wanaoichukia familia hiyo kutokana na kununua klabu yao.
Kambi ya pili ni ya washabiki ambao hawalii lakini wanawaasa wenzao kutulia kama waungwana. Wakawalaani wenzao wakisema si jambo la kawaida kwa mtu kufurahia kifo cha mwanadamu mwingine hata kama hawakuwa wakimpenda.
Kambi ya tatu ni ya washabiki ambao wanaonekana kukunjamana nyuso zao wakimlilia Glazer (85)  ambaye daima walikuwa wakimuunga mkono tangu aliponunua klabu 2005 kwa pauni milioni 790, wakisema chini yake palikuwa na mafanikio makubwa, ikiwa ni pamoja na ubingwa wa nchi mara tano na mara moja ule wa Ulaya.
Sir Alex Ferguson amekuwa akiwaunga mkono na kuwapinga washabiki waliokuwa wakiwachagiza Glazers, akisema ni watu wazuri ambao hawakuingilia kazi yake. Mwaka 2010 kulikuwa na maandamano na kutolewa kauli chafu dhidi ya mwekezaji huyo na familia yake kwenye dimba la Old Trafford.
Glazer hakupata kutia mguu wake Old Trafford na washabiki wanamkasirikia kwa madai kwamba aliisababishia klabu madeni makubwa yanayofikia pauni milioni 680 huku akichuma faida yeye na familia yake.
Haijajulikana athari za kifo hicho zitakuwa zipi kwa klabu, ikiwa ni miezi 11 tangu Kocha Ferguson aliyeiongoza klabu kwa miaka 26 ang’atuke na miezi kama hiyo tangu kocha aliyemrithi kwa makubaliano na Glazer, David Moyes afukuzwe kazi na chapa ya United kushuka thamani kimataifa.
cdt:tanzaniaspot.com

VIJANA MIAKA 15 TANZANIA WASHIKA NAFASI YA PILI AFRIKA

No Comments

Tanzania imeshika nafasi ya pili kwenye Michezo ya Afrika kwa Vijana (AYG) kwa upande wa mpira wa miguu kwa vijana wenye umri chini ya miaka 15 baada ya jana (Mei 29 mwaka huu) kuilaza Afrika Kusini mabao 2-0.


Mechi hiyo ilichezwa Uwanja wa SSKB jijini Gaborone ambapo kwa matokeo hayo Tanzania imetwaa medali ya fedha baada ya kushika nafasi ya pili. Nigeria ndiyo ilishika nafasi ya kwanza na kutwaa medali ya dhahabu.

Tanzania imemaliza ikiwa na pointi kumi ambapo ilishinda mechi tatu, sare moja na kupoteza moja mbele ya Nigeria.

Katika mechi ya kwanza ilitoka sare ya bao 1-1, ikawafunga Botswana 2-0, Swaziland wakachapwa 3-0 na baadaye kuwafunga Afrika Kusini 2-0. Timu ya Tanzania inayofundishwa na kocha Abel Mtweve ilifungwa na Nigeria mabao 2-0.

Wachezaji 16 waliounda kikosi hicho cha Tanzania katika michezo hiyo inayomalizika leo (Mei 30 mwaka huu) ni Adam Shayo, Amani Ally, Amos Manguli, Amri Nyuki, Amede Amani, Baraka Rashid, David Uromi, Goodlove Mdumule, Hance Msonga, Kelvin Kamalamo, Makalius Amrin, Nasson Chanuka, Paulo Ngowi, Petro Shaban, Rajab Mohamed na Thomas Chindeka.

Nchi nyingine zinazoshiriki michezo hiyo kwa upande wa mpira wa miguu ni Afrika Kusini, Botswana, Nigeria, Mali na Swaziland wakati Gabon na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) zilijitoa dakika za mwisho.
CDT: salehjembe blog
ETO'O AMTUNISHIA MISURI MOURINHO ATANGAZA KUJIUNGA ARSENAL

ETO'O AMTUNISHIA MISURI MOURINHO ATANGAZA KUJIUNGA ARSENAL

No Comments
20131115-091215.jpg

Eto’o aitaka Arsenal

By Israel Saria on May 29, 2014
*Asema Mourinho ni kibaraka
Mshambuliaji wa kati wa Cameroon, Samuel Eto’o ametangaza kutaka kujiunga na Arsenal ili amwoneshe Jose Mourinho kwamba bado wamo na amwaibishe watakapokutana.
Eto’o amekuwa katika majibizano na kocha wake huyo wa Chelsea, ambapo Mourinho amekuwa akimbeza kwamba hawezi kufunga mabao naye akamjibu kwa ishara uwanjani akiigiza kama mzee baada ya kufunga bao.
Eto’o amesema ana uwezo mkubwa wa kupachika mabao ambapo amedai kwamba kocha wake wa sasa, Mourinho ni kibaraka tu na hajui analolisema.
Mourinho alirekodiwa bila kujua akisema kwamba anadhani umri wa mshambuliaji huyo wa Simba Wasiofugika ni mkubwa kuliko inavyodaiwa, na majuzi Eto’o alimshambulia kocha huyo akisema ni mpuuzi.
“Wawakilishi wa Eto’o wameshaasiliana na Arsenal kuwajulisha kwamba mwanasoka huyo anaweza kupatikana kipindi hiki kama mchezaji huru hivyo wamchukue bila ada na kwamba kipaumbele chake namba moja ni kwenda Emirates,” mtu wa karibu na Eto’o amesema.
Eto’o mwenye umri wa miaka 32 amekuwa akidaiwa na Mourinho kwamba huenda anazidi miaka 35. Bosi wa zamani wa Eto’o katika timu ya taifa, Claude Le Roy amesema kwamba Eto’o amechukizwa sana na maneno ya Mourinho ya kumbeza.
Le Roy anasema kwamba Eto’o anaamini kwamba anaweza kufunga mabao mengi katika kipindi chote cha msimu na amedhamiria kuondoka Chelsea kwenda kuonesha ujuzi huo sehemu nyingine, hasa Arsenal.
“Uzuri wangu ni kwamba naweza kufunga mabao hata nikiwa na miaka 37 kwa sababu bado nina nguvu, uwezo na maarifa, si ajabu hata nikifikisha miaka 50 … hilo ndilo suala lililopo mezani wala si mambo ya Mourinho, nataka kujitoa kabisa kwa ajili ya timu na kuwasaidia kushinda vikombe.
“Kinyume na anachosema kibaraka huyo (Mourinho) juu ya umri wangu, bado nipo fiti kabisa na najihisi buheri wa afya. Nimethibitisha kwamba naweza kufanya vyema kuliko hata chipukizi,” akasema Eto’o ambaye anakwenda kwenye Kombe la Dunia kuwaongoza Cameroon.
Eto’o ndiye mshambuliaji wa kati wa Chelsea aliyefunga mabao mengi zaidi msimu uliopita (12) wakati wenzake Fernando Torres alifunga tisa na Demba Ba manane tu. Eto’o alifunga mabao matatu (hat-trick) dhidi ya Manchester United.
Kama atajiunga Arsenal atakuwa wa msaada mkubwa kushirikiana na Olivier Giroud na kusaidia mashambulizi na zaidi sana umaliziaji wa makini na kijanja, kitu ambacho Eto’o amethibitisha kuwa nacho.
TANZANIASPORT.COM
MINALA ANA MIAKA 17SIO 42

MINALA ANA MIAKA 17SIO 42

No Comments
20140529-135211-49931047.jpg

Minala ana miaka 17 si 42

By Israel Saria on May 29, 2014
Usoni mwake kuna alama au dalili za maisha yake ya nyuma, ambayo hayakuwa mazuri”
Hatimaye kitendawili cha umri wa msakata ndinga wa Lazio, Joseph Minala kimeteguliwa kwa kuhakikishwa kwamba umri wake ni miaka 17 si 42 iliyodaiwa na Tovuti ya Soka ya Afrika.
Kiungo huyo alikuwa akichunguzwa na Chama cha Soka Italia baada ya yeye kudai ana umri wa miaka 17 lakini usoni akaonekana kuwa na makunyanzi kama mtu aliyevuka sana umri huo. Wataalamu wanasema kwamba ‘uzee’ unaonekana usoni mwake kwa sababu ya maisha ya dhiki siku zilizopita.
Minala alizaliwa Cameroon na alijiunga na klabu hiyo ya jijini Roma msimu uliopita wa kiangazi na kuwachezea katika mashindano ya vijana Februari mwaka huu, huku watu wengi wakishangaa ikiwa kweli ni kijana.
Lazio walikuwa wametishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya yeyote aliyekwua akihoji uhalali wa mchezaji wao huyo kushiriki mashindano hayo na pia dhidi ya madai kwamba ana umri wa miaka 42, yaani miaka 25 zaidi ya umri wake halali.
Klabu hiyo imesema kwamba imepata hata cheti chake cha kuzaliwa ambacho walikipeleka kwenye chama cha soka na baada ya hapo watashughulika na yeyote atakayeendeleza propaganda za kumchafua kijana huyo juu ya umri wake.
Mtandao huo ulidai kwamba Minala alikiri kuwa umri wake wakati huo ulikuwa miaka 41 na hivyo sasa amefikisha 42 lakini yeye anakana kuzungumza na watu wa tovuti iliyotoa habari hizo.
“Usoni mwake kuna alama au dalili za maisha yake ya nyuma, ambayo hayakuwa mazuri. Ni hivyo tu. Hakuna kitu kingine chochote kinachoweza kumtonya mtu kwamba eti ana miaka zaidi ya 40. Ukiangalia kichwa chake ni cha kijana.
“Lakini acheza kwa kasi sana hata anapozungukwa na wachezaji wengi, mchezaji wa umri huo hangeweza kuwa na makeke kama huyu,” anasema mwanahabari Max Evangelista ambaye ni Mtaliano.
Minala anaelezwa kwamba ni yatima na aliishi maisha ya tabu sana mitaani nchini mwake kabla ya kupelekwa kituo cha watoto yatima kabla ya kubahatika kucheza soka barabarani kisha akapelekwa kwenye viwanja, akapanda chati hadi kupelekwa Italia.
TANZANIASPORT.COM
TAKUKURU WABISHA HODI UCHAGUZI WA SIMBA

TAKUKURU WABISHA HODI UCHAGUZI WA SIMBA

No Comments
By Israel Saria on May 29, 2014
*JULIO, MKWABI, WASOTA
*WAMBURA AKATA RUFAA
MAAFISA kutoka katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) jana waliivamia Kamati ya Uchaguzi ya Klabu ya Simba iliyokuwa inaendesha zoezi la usaili kwenye ukumbi wa Bwalo la Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuchukua nakala za vyeti na nyaraka nyingine zilizowasilishwa na wagombea uongozi wa klabu hiyo kwa ajili ya kuzifanyia uchunguzi.
Hatua hiyo imetokana na mmoja wa wagombea kuwasilisha taarifa katika taasisi hiyo kwamba baadhi ya wanachama wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi wanadaiwa kuwasilisha vyeti ‘feki’ na wengine wametoa rushwa kwa kamati ili wapitishwe hali ya kuwa hawana sifa zilizotajwa kwenye kanuni na katiba ya Simba.
Maafisa hayo kutoka TAKUKURU waliwasili kwenye ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi na kuanza kuzungumza na kamati hiyo na baada ya wao kuondoka saa 6:45 mchana, wajumbe walikaa kwa zaidi ya dakika 20 wakijadiliana na kabla ya kuendelea na zoezi hilo la kuwasaili wagombea.
Habari zilizopatikana jijini zinaeleza kuwa kamati hiyo huenda ikajiuzulu endapo italazimishwa kufanya maamuzi kinyume na kanuni na katiba ya Simba.
Pia kila mjumbe aliyekuwa anatoka katika usaili huo alieleza kwamba wanatakiwa kutoa ushirikiano kwa viongozi wa serikali watakapohitajika kufanya hivyo.
“Uchaguzi huu umeingiliwa na vyombo vya serikali, kwa hiyo endapo utatafutwa na vyombo hivyo uwe tayari kutoa ushirikiano,” aliliambia gazeti hili mmoja wa wagombea.
JULIO, MKWABI WASOTA
Wagombea wa nafasi ya Makamu wa Rais, beki na kocha wa zamani wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ na Swedy Mkwabi, ndiyo wagombea pekee waliohojiwa kwa muda mrefu na kamati hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti, Damas Ndumbaro.
Julio aliingia kwenye ukumbi wa usaili saa 4:58 asubuhi na kutoka saa 5:24 wakati Mkwabi ambaye alichelewa kufika katika usaili huo alihojiwa kwa dakika 33.
Hata hivyo zoezi hilo liliendeshwa bila ya kufuata herufi za wagombea katika nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji.
Andrew Tupa ndiyo alikuwa mgombea wa kwanza kuitwa kuanza kuhojiwa na kufuatiwa na Evans Aveva wote wanawania nafasi ya Urais wa klabu hiyo.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na kamati hiyo, kesho Ijumaa ndiyo siku ya kutangaza majina ya wagombea waliopita kwenye usaili huo kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Juni 29 mwaka huu.
WAMBURA AKATA RUFAA
Mgombea wa nafasi ya Urais wa Klabu ya Simba, Michael Wambura, leo Alhamisi amewasilisha rasmi rufaa katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) akipinga kuondolewa katika mchakato wa uchaguzi.
Wambura aliwasilisha pingamizi hilo na kueleza kwa kifupi kwamba ndani lina hoja 14.
Kamati ya Uchaguzi ya Simba ilitangaza kumuengua Wambura ikieleza kwamba si mwanachama halali kufuatia kusimamishwa na uongozi uliokuwa madarakani mwaka 2010.

WAMBURA AWASILISHA PINGAMIZI LAKE TFF

No Comments
WAMBURA AKIONYESHA PINGAMIZI LAKE NDANI YA OFISI ZA TFF, LEO.


Mgombea wa urais wa Simba, Michael Wambura leo wamewasilisha pigamizi lake la kuondolewa kwenye uchaguzi wa Simba.


Wambura amewasilisha pingamizi hilo kwenye ofisi za TFF katikati ya jijini la Dar es Salaam.
WAMBURA AKIWASILI KWENYE OFISI ZA TFF, LEO.

Wambura amesisitiza kuwa anachotaka haki ipatikane na anapingwa kuondolewa.
Kamati ya uchaguzi ya Simba inayoongozwa na mwanasheria na wakili maarufu nchini Dkt Damas Daniel Ndumbaro ilimuengua Wambura baada ya kugundua si mwanachama halali kutoka na kuondolewa mwaka 2010 baada ya kuipeleka Simba mahakamani.
MBEYA CITY FC KUUMANA NA UGANDA VICTORIA UNIVERSITY HATUA YA ROBO FAINALI

MBEYA CITY FC KUUMANA NA UGANDA VICTORIA UNIVERSITY HATUA YA ROBO FAINALI

No Comments
IMG_9441WAWAKILISHI wa Tanzania katika Michuano ya CECAFA Nile Basin Cup inayoendelea kushika kasi nchini Sudan, Mbeya City fc watachuana na Victoria University ya Uganda katika hatua ya robo fainali ya mashindano hayo.
Hizi hapa ndio mechi za robo fainali
Quarter final pairings
AFC Leopards [Kenya] VS Defence [Ethiopia]
Al Merreikh [Sudan] VS AcademieTchite [Burundi]
SC Victoria University [Uganda] VS Mbeya City [Tanzania]
Al AhliShandi [Sudan] VS Malakia [South Sudan]
TP MAZEMBE YAWAACHIA SAMATA, ULIMWENGU KUIONGEZEA NGUVU STARS

TP MAZEMBE YAWAACHIA SAMATA, ULIMWENGU KUIONGEZEA NGUVU STARS

No Comments
IMG_0750Klabu ya TP Mazembe imewaruhusu wachezaji wake Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu kujiunga na timu ya Taifa (Taifa Stars) ambayo tayari imewasili Harare, Zimbabwe kwa ajili ya mechi ya michuano ya Afrika.
Taifa Stars itacheza na Zimbabwe (Mighty Warriors) katika mechi ya marudiano raundi ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Morocco. Mechi hiyo itachezwa Jumapili (Juni 1 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa jijini Harare.
Samata na Ulimwengu watawasili Harare kesho (Mei 30 mwaka huu) saa 3.40 usiku kwa ndege ya Kenya Airways. Watajiunga na TP Mazembe mara baada ya mchezo huo ambapo Juni 2 mwaka huu watakwenda moja kwa moja Ndola, Zambia ambapo timu yao imepiga kambi kwa ajili ya mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika.
 BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
MICHUANO YA CECAFA YAINGIA ROBO FAINALI

MICHUANO YA CECAFA YAINGIA ROBO FAINALI

No Comments
Baadhi ya timu zitakazomenyana ni pamoja na Leopards ya Kenya, Al Merreikh na Al Sandy ambazo zinaongoza makundi yao
Mashindano ya kandanda ya kombe la Cecafa Nile Basin yanaingia robo-fainali Ijumaa na Jumamosi nchini Sudan huku timu mbili za Sudan, Al Merreikh na Al Shandy, na AFC Leopards ya Kenya zikiongoza makundi yao.
Al Merreikh na Victoria ya Uganda zilimaliza mechi zao za makundi na pointi saba kila mmoja lakini Merreikh ikaongoza kundi A kwa sababu ya wingi wa mabao.
Merreikh sasa itakutana na Academie ya Tchite Burundi ambayo Jumatano ilimeza bao 1-0 dhidi ya AFC Leopards ya Kenya, mfungaji akiwa ni Bernard Mangoli.
Victoria inapepetana na Mbeya City, Leopards dhidi ya Defence ya Ethiopia, Al Shandy inakwaruzana na jirani wao wa Sudan Kusini, Malakia.
Katika mechi za Jumatano, Leopards ilishangiliwa sana na baadhi ya wanafunzi wa Kenya wanaosomea Sudan pamoja na balozi wa Kenya nchini humo Abrown Suge na naibu wake Maurice Nakitare.
Leopards itakua bila wachezaji wake mhimu Allan Wanga, Jacob Keli, James Situma na Wycliffe Kasaya ambao wako na timu ya taifa Harambee Stars kwa mechi yao na Comoros Ijumaa ya kufuzu kwa fainali ya mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika.
Etincelles imerudi nyumbani bila ushindi, na hawatasahu mechi yao ya mwisho dhidi ya Mbeya City waliposhindwa kufunga penalti, huku Al Shandy ikiicharaza Defence mabao 2-0, wafungaji wakiwa ni Nadir Eltyab na Omar Mahmoud.
BBC
MKUTANO MKUU WA YANGA JUMAPILI

MKUTANO MKUU WA YANGA JUMAPILI

No Comments
Mkutano Mkuu wa Wanachama wa mabadiliko ya baadhi ya Vipengele kwenye Katiba utafanyika siku ya jumapili Juni Mosi 2014 katika Ukumbi wa Bwalo la Polisi - Oysterbay kuanzia majira ya saa 3 kamili asubuhi huku wanachama wote hai wa klabu ya Young Africans wakiombwa kujitokeza kwa wingi.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu, Afisa Habari wa Young Africans Bw Baraka Kizuguto amesema mkutano huo wa siku ya jumapili ni kwa ajili ya marekebisho ya katiba kama maagizo ya Shirikisho la Soka nchini TFF ilivyoagiza.
Jumapili tunafanya makutano wa marekebisho ya katiba lengo ni kuhakikisha wanachama wanapata nafasi ya kutoa maoni yao na kupitisha hivyo vipengele ambavyo vitapelekea Yanga kupeleka katiba yake TFF na kisha kwa msajili ili shughuli zote za klabu ziweze kufanyika kwa kufuata katiba mpya alisema Kizuguto.
Mara baada ya mabadiliko hayo nadhani tutakua tayari kuelekea kwenye mchakato wa Uchaguzi kwani tulikuwa tunasubiria marekebisho ya Katiba tu, TFF na msajili wakishaipitisha Katiba basi tutakua tayari kuelekea kwenye Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Viongozi.
Watakoruhusiwa kuhudhuria mkutano mkuu siku ya jumapili ni wanachama wa Yanga SC walio hai tu, kwa maana ambao wamelipia ada zao za uanachama mpaka kufikia kwa mwezi ujao wa Juni 2014.
Wanachama ambao bado hawajalipia Ada zao za uanachama wanaombwa kulipia mapema kabla ya siku ya mkutano, malipo yote yanafayika kwenye Idara ya Fedha makao makuu ya klabu kila siku muda wa kazi na siku ya jumamosi saa 3 asubuhi mpaka saa 7 mchana.
GPL
MBEYA CITY FC WATINGA ROBO FAINALI YA CECAFA NILE BASIN CUP MJINI KHARTOUM

MBEYA CITY FC WATINGA ROBO FAINALI YA CECAFA NILE BASIN CUP MJINI KHARTOUM

No Comments

 DSCF5413
MBEYA City imetinga Robo Fainali za michuano ya CECAFA Nile Basin Cup inayoendelea nchini Sudan baada ya  sare ya bila kufungana na Enticelles ya Rwanda usiku wa jana katika Uwanja wa Khartoum.
Matokeo hayo yanaifanya Mbeya City imalize hatua ya makundi kwa kujikusanyia  pointi nne baada ya mechi tatu, lakini ipo katika nafasi ya pili nyuma ya miamba ya soka nchini Kenya, AFC Leopards walioongoza kundi kwa pointi 9.

Mchezo wa mwingine wa usiku, AFC Leopard walishinda bao 1-0 dhidi ya Academie Tchite ya Burundi na kushinda kwa asilimia 100 katika kundi lao

FOOTBALL

ATHLETIC