TAIFA STARS YAIKUNG`UTA MALAWI

No Comments
DSC_45751Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Malawi katika mchezo wa kimataifa wa Kirafiki uliopigwa jioni ya leo Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Bao pekee la Stars limefungwa na kiungo mahiri, Amri Ramadhan Kiemba katika dakika ya 35 akimalizia kazi nzuri ya Shomary Kapombe.
Leo hii kocha wa timu wa Taifa Stars, Mholanzi Mart Nooij hakuanzisha kikosi chake kinachojulikana kuwa cha kwanza kwa lengo la kujaribu wachezaji wanaoweza kumsaidia katika mchezo wa marudiano dhidi ya Zimbabwe mjini Harare.
Kama ilivyokawaida, Nooij alimuanzisha mlinda mlango Deogratius Munish `Dida`, Himid Mao, Edward Charles, Said Mourad, Joram Mgezeke, Shomary Kapombe, Simon Msuva, Erasto Nyoni, Kevin Friday, Amri Kiemba na Khamis Mcha `Vialli`.
Katika kipindi hicho, Stars haikucheza vizuri sana tofauti na wapinzani wao Malawi ambao unaweza kusema walikosa bahati ya kufunga.
Kipindi cha pili, Nooij alibadilisha karibu kikosi chote ambapo wachezaji kama Kevin Yondan, Ramadhan Singano, Frank Domayo, Said Juma, Mwinyi Kazimoto.
Ushindi wa leo unatoa taswira nzuri kwa Stars kuelekea Harare ambapo wanaenda wakiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
Stars wanaotarajia kuondoka ijumaa Mei 30 mwaka huu kwa mujibu wa taarifa kutoka TFF, wanahitaji ushindi sare ya aina yoyote au ushindi ili kwenda sehemu inayofuata.
Aidha,  Afisa habari wa shirikisho la soka Tanzania Boniface Wambura Mgoyo amesema wameiandikia TP Mazembe wakiomba kuwapata wachezaji wawili wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu na kabla ya  ijumaa wanatarajia kupata majibu.

Dear readers, after reading the Content please ask for advice and to provide constructive feedback Please Write Relevant Comment with Polite Language.Your comments inspired me to continue blogging. Your opinion much more valuable to me. Thank you.