SOMA KWA KINA MAPINGAMIZI YOTE, YAKIWEMO YALIYOMNG’OA RICHARD WAMBURA

No Comments

DSC07072 copy

KAMATI YA UCHAGUZI SIMBA SPORTS CLUB
SAID RUBEYA, SWALEHE MADJAPA, USTADH M. HASSAN,
JACKSON J. SAGONGE & VALENTINE NYALU………………..……….. Waweka Pingamizi

DHIDI
MICHAEL RICHARD WAMBURA……………………………..…………Muwekewa Pingamizi
MAAMUZI

Waweka Pingamizi waliotajwa hapo juu, ambao ni wanachama wa Simba Sports Club wamemwekea pingamizi Mwekewa Pingamizi hapo juu kwa hoja zifuatazo:
i. Mwekewa Pingamizi aliipeleka Simba Sports Club mahakamani katika kesi Namba 100/2010 iliyofunguliwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es salaam, Kinyume na Ibara ya 11 (1) (e), (2), 12(3), na 55 ya Katiba ya Simba Sports Club ya Mwaka 2010.
ii. Mwekewa Pingamizi alisimamishwa Uanachama na Kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club iliyokutana tarehe 5 Mei 2010 na barua ya tarehe 6 Mei 2010, (Kumb. Na. SSC/MMKT/163/VOL.40/11) na hivyo basi anapoteza haki za kuwa mwanachama wa Simba Sports Club
iii. Mwekewa Pingamizi amekiuka Katiba ya Simba, TFF na FIFA kwa kuipeleka Simba Sports Club Mahakamani katika kesi Namba 100/2010.
iv. Mwekewa Pingamizi ameanza kampeni kabla ya muda wa Kampeni
v. Mwekewa Pingamizi amekiuka katiba ya Simba kwa kukubali uteuzi batili kuwa mjumbe kamati ya uchaguzi.
vi. Mwekewa pingamizi hana maadili ya Uongozi kwasababu alikiuka maadili akiwa kiongozi wa FAT/TFF.
vii. Mwekewa Pingamizi sio mwajibikaji.

Nakala ya mapingamizi hayo na mwaliko wa kikao cha kusikiliza pingamizi valikabidhiwa kwa mwekewa pingamizi tarehe 23 Mei 2014. Siku ya kusikiliza Pingamizi, tarehe 25 Mei 2014, Mwekewa pingamizi aliwasilisha mbele ya kamati ya uchaguzi “preliminary objections” mbili kama ifuatavyo:
i. Dhidi ya waweka pingamizi wote watano(ona kiambatanisho “A”)
ii. Dhidi ya Kamati ya Uchaguzi ya Simba (ona kiambatanisho “B”)

Kabla ya kuanza kusikiliza mapingamizi ya waweka pingamizi, kamati ilisikiliza “preliminary objections” na kutoa maamuzi kama ifuatavyo.
Mosi, “preliminary objections” dhidi ya wagombea watano (5), kimsingi ni majibu ya pingamizi toka kwa ya wakewa pingamizi, hivyo basi, hoja hizo zitapata fursa wakati mwekewa pingamizi anajibu hoja za waweka pingamizi.
Pili, “preliminary objections” dhidi ya kamati zinatupiliwa mbali kwa misingi ifuatavyo;
a. Uteuzi wa katibu wa kamati ya uchaguzi samba sports club ulifanywa na kamati ya utendaji ambayo mweka “prelimary objections” alihudhuria.
b. Kamati imeamua kuazima na kutumia kanuni za uchaguzi za TFF kwasababu Kamati ya utendaji Simba haijaandaa kanuni hizo.
c. Unapoazima na kutumia kanuni za Mamlaka nyingine sio lazima uzitumie kama zilivyo, una uhuru wa kufanya maboresha ili kuzingatia hali halisi ya Simba Sports Club.
d. Pingamizi dhidi ya Bw. Evans Aveva ni malalamiko ya kawaida ambayo Kamati inabidi iyazingatie kwa wakati wake na sio sehemu ya mapingamizi kwasababu muda wa pingamizi umekwisha.
e. Kanuni hazielezi haki ya kuweka “preliminary objections”, lakini kamati ilitumia busara kuzisikiliza.

Hivyo basi kamati ilitupilia mbali “prelimary objections” na kusikiliza pingamizi katika mfumo wa kawaida.
Kamati, awali ya yote, ilichambua masuala ya kimaadili na kuamua kuwa mambo hayo ya kimaadili, yapelekwe katika kamati ya maadili ya TFF na waweka pingamizi wenyewe. Mambo ya kupelekwa kamati ya maadili ni:
i. Mwekewa Pingamizi amekiuka katiba ya Simba kwa kukubali uteuzi batili kuwa mjumbe kamati ya uchaguzi.
ii. Mwekewa pingamizi hana maadili ya Uongozi kwasababu alikiuka maadili akiwa kiongozi wa FAT/TFF.
iii. Mwekewa Pingamizi sio mwajibikaji.

Kamati ilijadili na kuyatolea maamuzi mapingamizi yafuatayo:
i. Mwekewa Pingamizi ameanza kampeni kabla ya muda wa Kampeni.
Kamati ilikwisha toa adhabu ya ONYO KALI dhidi ya Mwekewa Pingamizi kuhusu kuanza kampeni kabla ya wakati, hivyo basi hawezi kuadhibiwa mara mbili kwa kosa ambalo ameshaadhibiwa.
ii. Mwekewa Pingamizi aliipeleka Simba Sports Club katika kesi Namba 100/2010 iliyofunguliwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es salaam, Kinyume na Ibara ya 11 (1) (e), (2), 12(3), na 55 ya Katiba ya Simba Sports Club ya Mwaka 2010.

Ushahidi uliotolewa mbele ya kamati unaonyesha kuwa Mwekewa pingamizi alifungua kesi No. 100/2010 katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu dhidi ya Simba Sports Club katika masuala ambayo hayapaswi kwenda mahakamani. Kitendo hicho ni ukiukwaji wa Ibara ya 11 (1) (e), (2), 12(3), na 55 ya Katiba ya Simba ya Mwaka 2010.
iii. Mwekewa Pingamizi alisimamishwa Uanachama na Kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club iliyokutana tarehe 5 Mei 2010 na hivyo basi anapoteza haki za kuwa mwanachama wa Simba Sports Club.
Kamati imepokea ushahidi na kuridhika kuwa tarehe 5 Mei 2010, kupitia kikao halali kamati ya utendaji ya Simba Sports Club ilimsimamisha Uanachama Mwekewa Pingamizi kwa tuhuma za kuipeleka Simba Mahakamani katika kesi tajwa. Baada ya kusimaishwa uanachama na kamati ya utendaji kwa mujibu wa Ibara 12(1),(2) & (3) ya katiba ya Simba mwaka 2010, jambo hilo lilipaswa kupelekwa katika mkutano mkuu ili mkutano mkuu, utoe adhabu au utoe msamaha. Kwa mujibu wa Katiba ya Simba, Ibara ya 55, adhabu ya kosa hilo ni kufukuzwa uanachama. Si kamati ya utendaji wala Mwekewa Pingamizi aliyepeleka suala hili katika mkutano mkuu ili litolewe uamuzi.
Kamati imepokea barua tatu, toka kwa Mwekewa Pingamizi, kuhusu uanachama wake Simba Sports Club. Barua ya kwanza iliandikwa tarehe 6 Novemba 2012 toka kwa Bw. Michael Wambura kwenda kwa Mwenyekiti wa Simba. Barua hiyo inakiri kosa la kuipeleka Simba makahamani na kuahidi kuwa hatarudia tena. Barua ya pili toka kwa Mwenyekiti wa Simba ya tarehe 15/09/2012, Ref. No. SSL/20/9/12, kukiri kupokea barua toka kwa Bw. Michael Wambura na kuahidi kuwa suala hilo litafanyiwa kazi, ingawa kamati ilibaini kuwa barua ya kujibu imeandikwa takribani miezi miwili kabla ya ile ya awali jambo ambalo haliwezekani. Barua ya tatu ni ya tarehe 25/9/1012, kumb. SSC 28/9/12 ambayo inasema samba haina tatizo na Bw. Michael Wambura, lakini Uhalali wa Barua hiyo unashaka kubwa sana kiasi cha kamati kuamua ipelekwe kwenye mamlaka husika kwa hatua zaidi.
Hivyo basi kamati imejiridhisha kuwa maamuzi ya Kamati ya utendaji ya tarehe 5 Mei 2010 ya kumsimamisha Mwekewa Pingamizi bado yanaendelea na yana nguvu za kisheria kwasababu hakuna maamuzi yoyote ya Mkutano Mkuu kubatilisha hatua hiyo.

Mwananchama ambaye amesimamishwa uananchama hana haki ya kushiriki katika shughuli za simba kwa mujibu wa Ibara ya 12 (3) ya Katiba ya Simba ya Mwaka 2010 na Ibara ya 12 (3) ya Katiba ya Simba ya Mwaka 2014.
iv. Mwekewa Pingamizi amekiuka Katiba ya Simba, TFF na FIFA kwa kuipeleka Simba Sports Club Mahakamani katika kesi Namba 100/2010.

Kamati inapenda kurejea maamuzi yake hapo juu katika suala ka kwenda mahakani kwa masuala ya Soka.
Hivyo basi Muwekewa Pingamizi, Bw. Michael Richard Wambura ameondolewa katika mchakato wa Uchaguzi, kwasababu zilizotajwa hapo juu.
Endapo upande wowote haujaridhika na maamuzi hayo, una haki ya kukata rufaa katika Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF.
Imetolewa tarehe 26 Mei 2014.
………………………………………………….
Dk. Damas Daniel Ndumbaro (PhD)
Mwenyekiti
Kamati ya Uchaguzi Simba Sports Club
KAMATI YA UCHAGUZI SIMBA SPORTS CLUB
ARTHUR MWAMBETA ……………………….………………..……….. Muweka Pingamizi

DHIDI
GEOFREY NYANGE (KABURU) ……………………………..…………Muwekewa Pingamizi

MAAMUZI
Awali, kamati ilipokea mapingamizi mawili dhidi ya Muwekewa Pingamizi toka kwa Bw. Hafidh Bashir na Bw. Arthur Mwambeta, lakini katika mchakato wa kusikiliza, Bw. Hafidh Bashir, aliamua kuondoa pingamizi hilo. Kwa mujibu wa maamuzi hayo tuna Muweka Pingamizi mmoja, tajwa hapo juu. Hoja za Muweka Pingamizi ni Kama ifuatavyo:
i. Muwekewa Pingamizi, akiwa sehemu ya Kamati ya Utendaji ya Simba kati ya Mwaka 2010-2013 alishindwa kuwasilisha Audited Accounts kwenye Mkutano Mkuu wa Simba, kwa mujibu wa ibara ya 19 (6), (7), 30 (1) (f) na 33 (5) ya katiba ya Simba ya Mwaka 2010.
ii. Muwekewa Pingamizi, akiwa sehemu ya Kamati ya Utendaji ya Simba kati ya Mwaka 2010-2013 alishindwa kujaza nafasi ya Mjumbe wa kamati ya Utendaji (Mwanamke) iliyowazi kwa mujibu wa Ibara ya 28(1)(c) na 29 (3) ya Katiba ya Simba ya Mwaka 2010.
iii. Muwekewa Pingamizi, akiwa sehemu ya Kamati ya Muda ya Simba Sports Club ya Mwaka 2005, aliuza gari la Simba Sports Club kinyume na maagizo ya Baraza la Wazee na Ibara ya 11(1) (b) na (c) na Ibara ya 6 (1) (iii) ya Simba.

Kamati ilisikiliza pande zote mbili na kuchambua ushahidi ulioletwa mbele yake na hatimaye kutoa maamuzi yafuatayo:
Hoja zote tatu za pingamizi hapo juu zinahusu tuhuma dhidi ya kamati ya utendaji ya Simba Sports Club na Kamati ya Muda ya Simba ya Mwaka 2005. Hakuna Ushahidi wowote dhidi ya mgombea binafsi. Kamati ya Uchaguzi haina mamlaka ya kuijadili na kuitolea maamuzi dhidi ya kamati ya utendaji kwasababu zifuatazo.
Mosi, Kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club ni Chombo cha juu kuliko kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club.
Pili, Kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club sio Mgombea, hivyo ipo nje ya Mamlaka ya Kamati ya uchaguzi.
Tatu, hakuna Ushahidi wowote dhidi ya Muwekewa Pingamizi binafsi na kama Ungekuwepo, basi suala hilo lingefikishwa katika kamati husika na sio kamati ya uchaguzi.

Hivyo basi Pingamizi, dhidi ya Muwekewa Pingamizi Bw. Geofrey Nyange (Kaburu) limetupiliwa Mbali.
Endapo upande wowote haujaridhika na maamuzi hayo, una haki ya kukata rufaa katika Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF.
Imetolewa tarehe 26 Mei 2014.
………………………………………………….
Dk. Damas Daniel Ndumbaro (PhD)
Mwenyekiti
Kamati ya Uchaguzi Simba Sports Club

 
KAMATI YA UCHAGUZI SIMBA SPORTS CLUB
SAID ALI MANERO ………………………………….………………..……….. Muweka Pingamizi

DHIDI
EVANS ELIEZA AVEVA ………….……………………………..…………Muwekewa Pingamizi

MAAMUZI
Kamati ilipokea mapingamizi dhidi ya Muwekewa Pingamizi, toka kwa Muweka Pingamizi hapo juu. Hoja za Muweka Pingamizi ni Kama ifuatavyo:
i. Muwekewa Pingamizi, aliwahi kugombea uchaguzi wa DRFA mwaka 2013 kwa jina la Evans Aveva lakini katika vyeti vyake anatumia jina la Evans Eliyeza, hivyo anaweza kuwa mtu tofauti, elimu ikwa haikidhi matakwa ya Katiba na uraia wake kutiliwa shaka, hivyo kuiuka ibara ya 26 (1) (2) ya Katiba ya Simba ya Mwaka 2010.
ii. Muwekewa Pingamizi, akiwa sehemu ya Kamati ya Muda ya Simba Sports Club ya Mwaka 2005, aliuza gari la Simba Sports Club kinyume na maagizo ya Baraza la Wazee na Ibara ya 11(1) (b) na (c) na Ibara ya 6 (1) (iii) ya Simba.

Kamati ilisikiliza pande zote mbili na kuchambua ushahidi ulioletwa mbele yake na hatimaye kutoa maamuzi yafuatayo:
Hati ya kusafiria ya Muwekewa Pingamizi namba AB 047458 iliyotolewa tarehe 26/08/2006 inamajina: Evans Elieza Aveva, hivyo hakuna utata wowote dhidi ya jina la mgombea. Muweka Pingamizi ameshindwa kuleta Ushahidi wowote kuhusu mashaka yake katika elimu, uanachama au uraia wa muwekewa pingamizi, hivyo basi hoja yake ya awali katika pingamizi hili inakosa miguu ya kikanuni na kutupiliwa mbali.
Hoja ya pili ya pingamizi hapo juu inahusu tuhuma dhidi ya Kamati ya Muda ya Simba ya Mwaka 2005. Hakuna Ushahidi wowote dhidi ya mgombea binafsi. Kamati ya Uchaguzi haina mamlaka ya kuijadili na kutoa maamuzi dhidi ya kamati ya muda ya Simba ya Mwaka 2005 kwasababu zifuatazo.
Mosi, Kamati ya Muda ya Simba ya Mwaka 2005, ambayo hivi sasa haipo, sio Mgombea, hivyo ipo nje ya Mamlaka ya Kamati ya uchaguzi.
Pili, hakuna Ushahidi wowote dhidi ya Muwekewa Pingamizi Binafsi na kama Ungekuwepo, basi suala hilo lingefikishwa katika kamati husika na sio kamati ya uchaguzi.

Hivyo basi Pingamizi, dhidi ya Muwekewa Pingamizi Bw. Evans Elieza Aveva limetupiliwa Mbali.
Endapo upande wowote haujaridhika na maamuzi hayo, una haki ya kukata rufaa katika Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF.
Imetolewa tarehe 26 Mei 2014.
………………………………………………….
Dk. Damas Daniel Ndumbaro (PhD)
Mwenyekiti
Kamati ya Uchaguzi Simba Sports Club
KAMATI YA UCHAGUZI SIMBA SPORTS CLUB
MWINYI SHARIFF DOSSI……………………….………………..……….. Muweka Pingamizi

DHIDI
SWEDI MKWABI, JOSEPH ITAN’GARE (KINESI)
SAIDI PAMBA, IBRAHIM MASOUD &
DANIEL MANEMBE ………………………………………………..…………Muwekewa Pingamizi

MAAMUZI
Kamati ilipokea pingamizi dhidi ya Wawekewa Pingamizi toka kwa Muweka Pingamizi tajwa hapo juu. Hoja za Muweka Pingamizi ni Kama ifuatavyo:
i. Wawekewa Pingamizi, wakiwa sehemu ya Kamati ya Utendaji ya Simba walifanya maamuzi ya kumpindua Mwenyekiti wa Simba Sports Club kinyume na ibara ya 33 (3) (a) (b) (c) na (d) ya katiba ya Simba ya Mwaka 2010.
ii. Wawekewa Pingamizi, wakiwa sehemu ya Kamati ya Utendaji ya Simba walishindwa kujaza nafasi zilizowazi ndani ya siku 90 kwa mujibu wa Ibara ya 28(1)(c) na 29 (3) ya Katiba ya Simba ya Mwaka 2010.

Muweka Pingamizi hakutokea bila sababu yoyote, hata hivyo, Kamati ilisikiliza utetezi wa wawekewa pingamizi na kuchambua ushahidi ulioletwa mbele yake na hatimaye kutoa maamuzi yafuatayo:
Hoja zote tatu za pingamizi hapo juu zinahusu tuhuma dhidi ya kamati ya utendaji ya Simba Sports Club. Hakuna Ushahidi wowote dhidi ya mgombea binafsi. Kamati ya Uchaguzi haina mamlaka ya kuijadili na kutoa maamuzi dhidi ya kamati ya utendaji kwasababu zifuatazo.
Mosi, Kamati ya Utandaji ya Simba Sports Club ni Chombo cha juu kuliko kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club.
Pili, Kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club sio Mgombea, hivyo ipo nje ya Mamlaka ya Kamati ya uchaguzi.
Tatu, Suala hilo linapaswa kupelekwa katika kamati husika ya maadili na sio kamati ya uchaguzi.

Hivyo basi Pingamizi, dhidi ya wawekewa Pingamizi wote hapo juu; SWEDI MKWABI, JOSEPH ITAN’GARE (KINESI), SAIDI PAMBA, IBRAHIM MASOUD &
DANIEL MANEMBE limetupiliwa Mbali.

Endapo upande wowote haujaridhika na maamuzi hayo, una haki ya kukata rufaa katika Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF.
Imetolewa tarehe 26 Mei 2014.
………………………………………………….
Dk. Damas Daniel Ndumbaro (PhD)
Mwenyekiti
Kamati ya Uchaguzi Simba Sports Club


KAMATI YA UCHAGUZI SIMBA SPORTS CLUB
JAMHURI MUSSA KIHWELO……………………….………………..……….. Muweka Pingamizi

DHIDI
SWEDI MKWABI, JOSEPH ITAN’GARE (KINESI)
SAIDI PAMBA, IBRAHIM MASOUD &
DANIEL MANEMBE ………………………………………………..…………Muwekewa Pingamizi

MAAMUZI
Kamati ilipokea pingamizi dhidi ya Wawekewa Pingamizi toka kwa Muweka Pingamizi tajwa hapo juu. Hoja za Muweka Pingamizi ni kama ifuatavyo:
i. Wawekewa Pingamizi, wakiwa sehemu ya Kamati ya Utendaji ya Simba walifanya kikao haramu kinyume na ibara ya 33 (4) ya katiba ya Simba ya Mwaka 2010 na kufanya mapinduzi dhidi ya Mwenyekiti.
ii. Wawekewa Pingamizi, wakiwa sehemu ya Kamati ya Utendaji ya Simba walipitisha maamuzi batili ya kuwafukuza walimu wa mpira bila malipo na mamlaka hivyo kusababisha usumbufu mkubwa hadi leo.

Muweka Pingamizi alitoa maelezo yake na wawekewa pingamizi walijibu hoja hizo. Kamati ilisikiliza hoja na kuchambua ushahidi ulioletwa mbele yake na hatimaye kutoa maamuzi yafuatayo:
Hoja za pingamizi hapo juu zinahusu tuhuma dhidi ya kamati ya utendaji ya Simba Sports Club. Hakuna Ushahidi wowote dhidi ya mgombea binafsi. Kamati ya Uchaguzi haina mamlaka ya kuijadili na kuitolea maamuzi dhidi ya kamati ya utendaji kwasababu zifuatazo.
Mosi, Kamati ya Utandaji ya Simba Sports Club ni Chombo cha juu kuliko kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club.
Pili, Kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club sio Mgombea, hivyo ipo nje ya Mamlaka ya Kamati ya uchaguzi.
Tatu, Suala hilo linapaswa kupelekwa katika kamati husika ya maadili na sio kamati ya uchaguzi.

Aidha kuhusu hoja ya Kufukuzwa Walimu wa mpira, kamati inamshauri muweka pingamizi apeleke shauri hilo katika Kamati ya Sheria ya TFF au Mahakama ya kazi kwasababu ni suala la mwajiri na mwajiriwa.
Hivyo basi Pingamizi, dhidi ya wawekewa Pingamizi wote hapo juu; SWEDI MKWABI, JOSEPH ITAN’GARE (KINESI), SAIDI PAMBA, IBRAHIM MASOUD &
DANIEL MANEMBE limetupiliwa Mbali na yale yanayohusu maadili yaenda katika kamati husika.

Endapo upande wowote haujaridhika na maamuzi hayo, una haki ya kukata rufaa katika Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF.
Imetolewa tarehe 26 Mei 2014.
………………………………………………….
Dk. Damas Daniel Ndumbaro (PhD)
Mwenyekiti
Kamati ya Uchaguzi Simba Sports Club
KAMATI YA UCHAGUZI SIMBA SPORTS CLUB
ARTHUR MWAMBETA ……………………….………………..……….. Muweka Pingamizi

DHIDI
SWEDI MKWABI…………………………………………………………Muwekewa Pingamizi

MAAMUZI
Muweka Pingamizi aliondoa pingamizi lake. Hivyo kamati haikusikiliza pingamizi hilo.
Imetolewa tarehe 26 Mei 2014.
………………………………………………….
Dk. Damas Daniel Ndumbaro (PhD)
Mwenyekiti
Kamati ya Uchaguzi Simba Sports Club

 
KAMATI YA UCHAGUZI SIMBA SPORTS CLUB
LUKA NGWAKO MBAPILA……………………….………………..………..} Waweka Pingamizi
OMAR JUMA MUNGA …………………………………………………………}
SALIM R. SIMBA …………………………………………………………………}
ABDALLAH MKOVA ……………………………………………………………}

DHIDI
SWEDI MKWABI…………………………………………………………Muwekewa Pingamizi

MAAMUZI
Waweka Pingamizi wote walileta hoja zifuatazo.
i. Wawekewa Pingamizi, wakiwa sehemu ya Kamati ya Utendaji ya Simba walishindwa kujaza nafasi zilizowazi ndani ya siku 90 kwa mujibu wa Ibara ya 28(1)(c) na 29 (3) ya Katiba ya Simba ya Mwaka 2010.
ii. Taarifa za mahesabu kwenye mkutano mkuu ziliwasilishwa kwa lugha ya kiingereza hivyo kumnyima haki ya kujua mapato ya klabu kwa miaka minne.

Waweka Pingamizi hawakutokea bila sababu yoyote, hata hivyo, Kamati ilisikiliza utetezi wa wawekewa pingamizi na kuchambua ushahidi ulioletwa mbele yake na hatimaye kutoa maamuzi yafuatayo:
Hoja zote tatu za pingamizi hapo juu zinahusu tuhuma dhidi ya kamati ya utendaji ya Simba Sports Club. Hakuna Ushahidi wowote dhidi ya mgombea binafsi. Kamati ya Uchaguzi haina mamlaka ya kuijadili na kuitolea maamuzi dhidi ya kamati ya utendaji kwasababu zifuatazo.
Mosi, Kamati ya Utandaji ya Simba Sports Club ni Chombo cha juu kuliko kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club.
Pili, Kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club sio Mgombea, hivyo ipo nje ya Mamlaka ya Kamati ya uchaguzi.
Tatu, Suala hilo linapaswa kupelekwa katika kamati husika ya maadili na sio kamati ya uchaguzi.

Hivyo basi pingamizi linatupiliwa mbali.
Kwakuwa hawakuja kutetea pingamizi lao hawana haki ya kukata rufaa.
Imetolewa tarehe 26 Mei 2014.

………………………………………………….
Dk. Damas Daniel Ndumbaro (PhD)
Mwenyekiti
Kamati ya Uchaguzi Simba Sports Club


KAMATI YA UCHAGUZI SIMBA SPORTS CLUB
MWINYI SHARIFF DOSSI……………………….………………..………..} Waweka Pingamizi
SWALEHE MADJAPA ……………………………………………………….}

DHIDI
KARAHA HASSAN CHANO (ALMAS)………………………………………Muwekewa Pingamizi

MAAMUZI
Waweka Pingamizi wote walileta hoja zifuatazo.
i. Muwekewa Pingamizi, wakiwa sehemu ya Kamati ya Utendaji ya Simba (Mhasibu Msaidizi) hakuleta taarifa za fedha katika Mkutano Mkuu ambayo ilisababisha kuondolewa katika uchaguzi wa 2010 baada ya kuwekewa pingamizi na Asha Kigundula na hajawahi kusamehewa na mkutano mkuu wowote.

Waweka Pingamizi hakutokea bila sababu yoyote, hata hivyo, Kamati ilisikiliza utetezi wa wawekewa pingamizi na kuchambua ushahidi ulioletwa mbele yake na hatimaye kutoa maamuzi yafuatayo:
Hoja zote tatu za pingamizi hapo juu zinahusu tuhuma dhidi ya kamati ya utendaji ya Simba Sports Club. Hakuna Ushahidi wowote dhidi ya mgombea binafsi. Kamati ya Uchaguzi haina mamlaka ya kuijadili na kuitolea maamuzi dhidi ya kamati ya utendaji kwasababu zifuatazo.
Mosi, Kamati ya Utandaji ya Simba Sports Club ni Chombo cha juu kuliko kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club.
Pili, Kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club sio Mgombea, hivyo ipo nje ya Mamlaka ya Kamati ya uchaguzi.
Tatu, Suala hilo linapaswa kupelekwa katika kamati husika ya maadili na sio kamati ya uchaguzi.

Hivyo basi pingamizi linatupiliwa mbali.
Kwakuwa hawakuja kutetea pingamizi lao hawana haki ya kukata rufaa.
Imetolewa tarehe 26 Mei 2014.

………………………………………………….
Dk. Damas Daniel Ndumbaro (PhD)
Mwenyekiti
Kamati ya Uchaguzi Simba Sports Club


Chanzo: salehjembe.blogspot.com

Dear readers, after reading the Content please ask for advice and to provide constructive feedback Please Write Relevant Comment with Polite Language.Your comments inspired me to continue blogging. Your opinion much more valuable to me. Thank you.