NIGERIA WAICHAPA AMAVUBI

No Comments
Timu ya taifa ya soka ya akina mama wa Nigeria ‘Super Fulcon’ wakichezea ugenini wameifunga Timu ya taifa la Rwanda kwa mabao manne kwa moja.
Mchuano huo ulionekana kutawaliwa na akina mama wa Nigeria kwa ushindi ambao washindani wameafiki bila ya ubishi.

kipindi cha kwanza kilimalizika Nigeria Super Fulcon ikiongoza kwa mabao matatu kwa bila.Super Fulcon walianza mchezo kwa kasi wakionekana kuwa na kiu ya kupata ushindi ambapo mnamo dakika ya nane walizitingisha nyavu za timu ya soka ya kina mama wa timu ya Amavubi kwa kujipatia bao la kwanza.

Mnamo kipindi cha pili cha mchezo , Wanawake wa Amavubi walijikakamua na kushambulia Super Fulcon iliyosababisha kupata goal Kick iliyopigwa vema na mshambuliaji wa mbele Clemantine,na kuishia katika nyavu za lango la Super Fulcon na kuandika bao la kwanza.
Muda mfupi kabla ya mchuano kumalizika timu ya akina mama wa Super Fulcon walipata penalti ambayo bila mzaha iliingia vema katika nyavu za lango la Amavubi na matokeo kuwa mabao manne kwa moja la kufuta machozi ya Amavubi.
'Rwanda ilijitahidi kadri ya uwezo wao'
Aziza Ashoala wa Super Fulcon ndiye alikuwa nyota wa mchezo huo kwa kuipatia Nigeria mabao mawili.
Kocha wa timu ya ya taifa ya akina mama Grace Nyimawumuntu alikiri kushindwa akibaini kwamba wametumia mbinu na uwezo wote walio kuwa nao.
"Hakika haikuwa rahisi kamwe hata nanyi mliokuwa hapa mmeshuhudia kwanza timu tuliyocheza nayo iko katika kiwango cha bora kabisa.Inauzoefu wa mashindano na ina nguvu,Umeona kwamba wakati umefika tukaonekana dhaifu yaani kasi yetu ilikuwa ndogo sana,ukiangalia mabao yote tuliyofungwa,yametokana na kasi ndogo,’’ alisema Nyimawumuntu
Amavubi wanawake walifikia ngazi hii baada ya ushindi dhidi ya timu ya akina mama wa Kenya.
Mchuano wa marudio Ugenini Amavubi mnamo wiki mbili zijazo.
Fainali za michuano ya timu ya mataifa ya akina mama barani Afrika inatazamiwa kufanyika mwezi wa Novemba mjini Vindhouk Namibia.Super Fulcon,ya Nigeria ni bingwa mtetezi wa kombe hilo mara nane.

Dear readers, after reading the Content please ask for advice and to provide constructive feedback Please Write Relevant Comment with Polite Language.Your comments inspired me to continue blogging. Your opinion much more valuable to me. Thank you.