KUENGULIWA KWA WAMBURA KWAIBUA MAPYA SIMBA MZEE KINESI AJITOA KWENYE KINYANG'ANYIRO

No Comments
10277611_727071024023512_2058992934153653762_nMzee Kinessi (kushoto) akiwa na mgombea mwingine wa nafasi ya makamu wa rais, Geofrey Nyange Kaburu
………………………………………………
SIKU moja tu baada ya kamati ya uchaguzi ya klabu ya Simba sc chini ya mwenyekiti wake, Wakili Dkt. Ndumbaro, kumuengua mgombea wa rais wa klabu hiyo, Michael Richard Wambura, katika uchaguzi wa juni 29 mwaka huu, mgombea wa nafasi ya umakamu wa rais, Joseph Itang`are `Mzee kinesis` amejitoa katika kinyang`anyiro hicho.
Kinessi ambaye ni kaimu mwenyekiti wa Simba sc na mjumbe wa kamati ya utendaji katika uongozi unaomaliza muda wake chini ya mwenyekiti wake Ismail Aden Rage amejiondoa kwasababu ya Wambura kutotendewa haki na kamai ya uchaguzi.
Ili kuudhihirishia Umma kuwa hajaunga mkono kitendo cha Wambura kuenguliwa, Kinessi amesema hataenda kwenye zoezi la usaili linalotarajiwa kuanza hapo kesho.
Mzee Kinnessi anaamini Wambaru ameonewa na kwakuwa na yeye ni miongoni mwa viongozi waliopo madarakani, hataki kuonekana kama yupo nyuma ya njama za kumuondoa mgombea huyo kipenzi kwa wanachama wengi wa Simba.
Aidha, amedai Wambura ni mtu anayeungwa mkono na watu wengi ambao hawajaridhishwa na matokeo ya mapingamizi juu yake, hivyo wanahitaji kufafanuliwa zaidi na kamati ya uongozi.
Leo mchama, mamia ya wanachama wa Simba walijikusanya na kuandamana makao makuu ya klabu ya Simba, maeneo ya Msimbazi Kariokoo, jijini Dar es salaam na kuzuia barabara kwalengo la kuhitaji ufafanuzi juu ya kuondolewa kwa Wambura.
Haya hapa chini ni mapingamizi aliyowekewa Michael Richard Wambura na matokoe yake kusomwa jana na mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi.
SHAFFI

Dear readers, after reading the Content please ask for advice and to provide constructive feedback Please Write Relevant Comment with Polite Language.Your comments inspired me to continue blogging. Your opinion much more valuable to me. Thank you.